Friday, 14 April 2017
Heri ya Ijumaa kuu kwa wakristu wote!!
Leo hii April 14, ni siku ya Ijumaa kuu ambapo wakristu duniani kote wanafanya kumbukumbu ya mateso na hatimaye kifo cha bwana wetu Yesu krisru zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Katika makanisa mbalimbali wakristu wamejitokeza kwaajili ya ibada takatifu, kubwa zaidi ikiwa ni kukumbuka mateso ya Muumba wao lakini pia ni wasaa wa kuweza kutafakari mema yote ambayo mwenyezi mungu amewatendea.
Nimatumaini yangu pia ni nafasi ya kuwakumbuka wahitaji mbalimbali wenye shida za aina mbalimbali kama wagonjwa, watu ambao nchi zao zipo katika vita, wenye ukosefu wa chakula, maji, yatima wote, na wahitaji wa kila namna.
Ukiwa ni Mkristu kwakuwa kiongozi wa ukristu duniani aliimiza upendo, amani msamaha ni wakati sasa kwa wewe uliye mkristu kujaribu kuishi maagizo ya Yesu Kristu kwasababu ndiyo maelekezo yake yalivyo tuishi hivyo katika dunia hii.
Niwakati wa kuwa chanzo cha amani na mpatanishi pale ambapo amani imetoweka lakini kubwa zaidi ni kuwaza maisha yako baada ya kuondoka katika dunia hii.
rukwakwanza.blogspot.com inakutakia heri ya Ijumaa kuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment