INYONGA KUMUONA RAIS MAGUFULI
Gurian Adolf
WAKAZI wa kijiji cha
Inyonga wilaya ya mlele mkoani Katavi wamedai kuwa wanafunga safari na kwenda
Ikulu kwa lengo la kumuona Rais John
Magufuli ili kumueleza kuchoshwa na umasikini ambao serikali imewasasabisha
kutokana na kushindwa kuwalipa fedha za fidia.
Walimueleza hayo mkuu wa
wilaya hiyo Said Njiku wakidai kuwa
wamesubiri kwa takribani miaka minne sasa bila mafanikio licha ya kwamba
walihakikishiwa wangelipwa fedha hiyo ndani ya muda mfupi.
Akizungumza kwa niaba ya
wenzake Fransi Jerememia alisema kuwa wakati wilaya hiyo inaanzishwa wakazi hao
waliombwa watoe eneo la ardhi ambalo walikuwa wakiishi,kulima na kufuga ili
serikali ijenge hospitali ya wilaya kwa makubaliano ya kulipwa fidia lakini
suala hilo limekuwa ni adhabu kwao.
Alisema kuwa baada ya
kukubali ombi hilo la serikali waliambiwa waache kufanya ujenzi,kilimo,ufugaji
na shughuli nyingine kwani watapewa fidia ili wakatafute maeneo mengine lakini
hali imekuwa ni tofauti mpaka sasa wanaishi maisha ya dhiki kutokana na
kutokuwa na ardhi.
‘’tulitegemea tungelipwa
fidia ndipo tungeenda kununua ardhi ili tujenge na kuendelea na maisha yetu
huko lakini mpaka sasa hakuna kinachoeleweka kwa hivyo tumechoka sasa ni kwenda
kumuona rais tu ndiyo tunaamini atatusaidia serikali ya wilaya imeshindwa
kabisa’’….alisema.
Naye Maria Simwanza mkazi
wa kijiji hicho alisema kuwa mpaka sasa wamekwisha changishana fedha kiasi cha
shilingi 800,000 fedha ambazo zitatumika
kama naauri na kujikimu watu ambao watakwenda kumuona raisi kwani wanaishi
maisha ya dhiki huku wakisikitika kuwa serikali ndiyo inayowatesa kwa kiwango
hicho.
Alisema pamoja na kuwa mkuu
wao wa wilaya ameahidi atalishughulikia suala hilo wamedai kuwa kila mara
amekuwa akiwapa majibu ya kisiasa ambayo pia wameyachoka iliyobaki ni kumuona
raisi tu huenda yeye atapatia ufumbuzi suala hilo kwani wanazidi kuwa masikini
wa kutupa kutokana na kutokuwa na ardhi.
Hata hivyo mkuu huyo wa
wilaya ya Mlele Said Njiku aliwasihi wananchi hao kuwa wavumilivu pamoja na changamoto
hizo lakini wanapaswa kutambua kuwa serikali itawalipa na tatizo hilo
litakwisha kabisa.
mwisho
No comments:
Post a Comment