Na Gurian Adolf
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa Hamidu
Njovu amewaonya baadhi ya wakazi wa manispaa hiyo kuacha tabia ya kupuuza sheria
ndogo zinazotungwa na halmashauri hiyo kwani ipo siku tabia hiyo itawatokea
puani.
Akizungumza na gazeti hili mkurugenzi huyo alisema kuwa wapo
baadhi ya watu kwa makusudi wakijua kuwa kunabaadhi ya vitu vinakatazwa na
sheria ndogo za manispaa hiyo lakini wanakiuka makusudi bila hofu ya
kuchukuliwa hatua.
Akitolea mfano amesema kuwa moja ya sheria hizo ni suala la
usafi kwa kila mkazi wa manispaa hiyo lakini wapo baadhi ya watu wamekuwa na
tabia ya kutapisha vyoo,kufanya biashara katika mazingira machafu bila kuwa na
hofu ya sheria pamoja usalama wa afya zao.
Mkurugenzi huyo wa Manispaa amesema kuwa tayari ametoa
maagizo kwa watendaji wa halmashauri hiyo kusimamia suala la usafi ili
kuepukana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwani jitihada zisipofanyika
ugonjwa huo unaweza kulipuka katika manispaa hiyo.
Aidha Njovu aliwataka vijana katika msimu huu wa kilimo
kujishughulisha ili nyakati za mavuno weweze kupata mazao mengi ambayo
yatawasaidia kupiga hatua katika maisha yao na familia zao.
Alisema vijana wanapaswa kutambua kuwa kunasheria ya nguvu
kazi ambayo sasa imefika wakati lazima isimamiwe ipasavyo kwani wapo vijana
wanaoshinda kijiweni bila kuzalisha huku wakiona mvua zinaendelea kunyesha na
wao wamekuwa wakwanza kulia ugumu wa maisha.
Ameongeza kuwa huu ni wakati wa kutekeleza kaulimbiu ya Rais
John Magufuli ya 'Hapa kazi tu" hivyo vijana hawanabudi kubadirika na
kufanya kazi kwa bidii tofauti na hivyo watabaki wakililia ugumu wa maisha siku
zote.
No comments:
Post a Comment