Saturday, 7 December 2013

WANAWAKE WATAKIWA KUTOWAOGOPA WAUME ZAO

WANAWAKE mkoani Rukwa wameshauriwa kuacha tabia ya kuwaogopa waume zao kama kweli wanania ya dhati ya kupambana na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia mkoani humo.

Hayo aliyasema jana na kaimu mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyeka wakati akihutubia katika mkutano wa kuzindua baraza la kupinga unyanyasaji wa kinsia mkoani humo lilofanyika katika shule ya msingi Chanji inayotoa elimu jumuishi kwa wanafunzi wote mkoani humo.

 Alisema kuwa moja kati ya sababu zinazochangia kuendele na kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake mkoani humo ni tabia ya wanawake kuwaogopa waume zao kutoka na kuwa iwapo mwanamke anakwenda kumshitaki mume wake polisi akirejea nyumbani hujikuta anapokea kipigo na pengine hata kuachika katika ndoa yake.

 Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kuktokana na kipigo hicho wengi wa wanawake wamekuwa wakinyanyasika,kudhulumika na kutendewa vitendo vingi vibaya lakini wamekuwa wakikaa kimya bila kutoa taarifa polisi wakiogopa kupigwa na waume zao.

Alisema iwapo wanawake hao hawapendi unyanyasaji huo wanapaswa kuacha uoga na wawe wanatoa taarifa polisi ili wanaume hao wawe wanachukuliwa hatua za kisheria na kwa mwanamke atakayetoa taarifa lazima polisi wampe ulinzi wa kutosha ili kumuepushia vitisho na kipigo kutoka kwa mume wake huyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa wanawake aliyehudhuria uzinduzi huo Monica Machulo alisema kuwa tatizo kubwa linalosababisha wanawake wengi kunyanyasika katika ndoa zao mkoani Rukwa ni kutokuwa na mgawanyo sawa wa lasilimali za familia ambapo wanaume wamekuwa wakizitumia vibaya peke yao bila kuihusisha familia.

 Alisema wakati wa uzalishaji hususani wakati wa kulima familia nzima imekuwa ikihusika bila kutegea lakini baada ya mavuno mahindi yote yanakuwa chini ya baba wa familia na wengi wao wamekuwa wakiuza bila kuihusisha familia na kutumia fedha zote peke yake katika anasa na iwapo mama wa nyumba anapomuuliza baba ndipo matatizo yanapoanza na kusababisha unyanyasaji katika famili na pengine hupelekea hata mauaji kutokana na kupigana mara kwa mara.

No comments: