Tuesday, 17 December 2013
TCCIA RUKWA YAOMBA MBOLEA AINA YA DAP
MWENYEKITI wa chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo TCCIA mkoani
Rukwa Shadrack Malila ameiomba serikali kuwashauri wakulima wa mkoa
huo kutumia mbolea nyingine ya kupandindia mahindi tofauti na mbolea
ya minjingu kwani mbolea hiyo haijafanyiwa utafiti katika mkoa huo na
imekuwa ikiwasababishia wakulima hasara kubwa kutokana na kukosa
mazao.
Hayo ameyasema hivi karibuni wakati alipoitisha mkutano na waandishi
wa habari ofisini kwake kwania ya kuiomba serikali kutopeleka mbolea
ya ruzuku aina ya minjingu katika mkoa huo kwani imekuwa
ikiwasababishia wakulima kutopata mazao ya kutosha hivyo kutokuwa na
tija kwa wakulima hao.
Alisema kuwa tangu awali wakulima hao wamekuwa wakiikataa mbolea hiyo
kwani walipoanza tu kuitumia kwa kupandia imekuwa haistawishi mahindi
vizuri tofauti na mbolea ya DAP ambayo inaonekana kustawisha mahindi
vizuri na wakulima wamekuwa wakiitumia hasa ukizingatia serikali
ilikuwa ikitoa kwa ruzuku.
Katika msimu huu wa kilimo serikali inanatoa ruzuku mbolea ya minjingu
ambayo wakulima wamekuwa wakikataa kuitumia kutokana na kutofanya
vizuri hivyo chama cha biashara viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Rukwa
inaiomba serikali kutoa mbolea ya DAP katika ruzuku kama wanavyopewa
wakulima wa mikoa ya kaskazini ili wakulima wa mkoa wa Rukwa nao
wapate mazao ya kutosha.
Mwenyekiti Malila alisema pia serikali ijitahidi kuwalipa madeni
wakulima iliyokopa mahindi kwani wengi wao wanategemea fedha hizo
hususani katika kipindi hiki cha masika ambapo mvua zimeanza kunyesha
kwani wengi wao wanategemea kuanza kulima na kununua mbolea kutokana
na fedha hizo.
Alisema kuwa kutokana na serikali kutolipa madeni kwa wakulima hao
wengi wao wamepata shida ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto wao kwa
shida maisha ya dhiki,matibabu yasiyokuwa ya kiwango kizuri na taabu
nyingine nyingi kwani walikuwa wakitegemea fedha hizo ili wajikimu
katika maisha yao lakini hali imekuwa ni tofauti.
Malila alisema kuwa mkulima wa mkoa wa Rukwa anaisha maisha ya shida
kanakwamba hana kitu kumbe tatizo ni serikali ndiyo iliyosababisha
hali ngumu kwa mkulima huyo ambaye anategemea kipato kutokana na
biashara ya mazao ambapo aliiuzia serikali akiamini kuwa atapata fedha
zake mapema lakini hali imekuwa kinyume na matarajio yake.
Wakulima mkoani Rukwa wanaidai serikali zaidi ya shilingi bilioni 10
ambazo zimetokana na serikali kuwakopa tani elfu 20 za mahindi fedha
ambazo wanazihitaji kwaajili ya kutumia katika mahitaji yao mbalimbali
ikiwemo katika kilimo cha msimu huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment