Sumbawanga
SERIKALI mkoani Rukwa imewataka wananchi wanaoishi katika vijiji vilivyopo mipakani kuacha kuwapokea kiholela watu wanaoingia nchini hata kama ni ndugu zao kwani kufanya hivyo wanahatarisha usalama wa wananchi wengine.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alitoa agizo hilo jana wakati akihutubia wananchi wa kijiji cha Kipwa kilichopo mwambao mwaziwa Tanganyika wilayani Kalambo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.
Alisema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi ya kuwapokea wageni kutoka katika nchi za Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nakuwapa hifadhi kikinyume na sheria kwa madai kuwa wana undugu na watu hao.
Wangabo alisema kuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakipokelewa na kupewa mpaka uongozi katika serikali za vijiji kitendo mbacho ni hatari kwani wanahatarisha usalama wa nchi.
Alisema kuwa serikali haikatai wageni kuingia nchini lakini ni wanapaswa wafuate taratibu za nchi tofauti na hapo nilazima wachukuliwe hatua za kisheria hata kama wanakuja kuwasalimia ndugu zao.
"naagiza kuwa nimarufuku kuwapokea wageni na kuwapa hifadhi hata kama mna udugu, mmeoa na kuolewa katika nchi zao ni lazima sheria za nchi zifuatwe vinginevyo watachukuliwa hatua tambueni ni makosa kuingia katika nchi nyingine bila kufuata utaratibu" alisema
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi wanaoishi mipakani kudumisha amani na mshikamano kwani kumekuwa na mivutano ya mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kugombania maeneo ya kuvua Samaki kwani kila wananchi wafanye shughuli katika nchi yao.
Alisema nikosa raia wa nchi moja kwenda kufanya shughuli za uvuvi katika eneo la nchi nyingine kwani kila mahali kunasheria na taratibu zake hivyo atakayekamatwa atachukuliwa hatua kwa kukiuka sheria hizo.
Hata hivyo mmoja wa wakazi wakijiji hicho Maria Simzosha Aliiomba serikali ya mkoa kupitia maliasili kuwasaidia kukabiliana na mamba waliopo katika eneo la kijiji hicho cha Kipwa kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika kwani wananchi wamekuwa wakiliwa na mamba mara kwa mara.
Mwisho
No comments:
Post a Comment