Na Gurian Adolf
Nkasi
TAASISI ya utafiti na udhibiti wa viuatilifu TPRIimeyafungia maduka mawili yanayouza viuatilifu katika kata ya kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa baada ya kukiuka sheria zinazowaelekeza kwa mujibu wa vibali vyao baada yakubainika wakiuza mbolea kwa kupima mwenye vikombe huku mifuko ya mbolea hiyo ikiwa haina lebo maalumu ya ubora.
Tasisi hiyo imewafungia wafanyabiasha hao baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza na kukuta maduka hayo yakiuza mbolea kinyume cha sheria na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo kutokana na kukikuka kanuni za kuuza madawa kama walivyoelekezwa kisheria.
Mkaguzi mwandamizi wa TPRI kanda ya Dar es salaam, Samwel Mmari aliyataja maduka yaliyofungiwa kuwa ni duka la Pembejeo shop mali ya Paul Kakubwa na duka la Samwel Ntiha ambao wote wamekutwa na hatia ya kufanya biashara kinyume na sheria ya udhibiti wa viuatilifu namba 30 ya mwaka 1997.
Alisema kuwa pia wauzaji wa maduka hayo wamekuwa wakiuza huku hawajapata mafunzo maalumu ya kuuza maduka ya pembejeo ikiwa ni pamoja na kuuza pembejeo za kilimo kwa kupima kwenye vikombe na mifuko ya pembejeo zinazouzwa haina lebo ya ubora huku bidhaa nyingine zikiwa hazina alama ya uthibitisho ya TPRI.
Mmari alisema kuwa bidhaa zote zisizo na lebo na zinazouzwa kwa kupima kwenye vikombe na zile zisizo na alama ya TPRI waliamua kuzichukua na watazipeleka makao makuu kwa ajiri ya kuzitekeza.
Aliwataka wamiliki wa maduka ya pembejeo kufuata sheria kanuni na taratibu zinazowaelekeza wao kuuza maduka hayo kinyume cha hapo ni kosa kisheria na kuwa kwa kufanya hivyo wakifikishwa mahakamani nakupata adhabu ikiwemo kulipa faini hadi yashilingi milioni 10 au kifungo cha miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja.
Kwa upande wake kaimu afisa kilimo wa wilaya hiyo Japhet Kamwela aliwasisitiza wafanyabiashara ya pembejeo kutii sheria na kufuata maelekezo ya wataalamu waliyopewa na ofisi yao na pia aliwaagiza wataalamu wa kilimo ngazi za vijiji na kata kupita kila wakati kukagua maduka yanayouza pembejeo za kilimo ili kuhakikisha wanafanya biashara kwa kuzingatia matakwa ya kisheria.
Mwisho
No comments:
Post a Comment