Na Gurian Adolf
Nkasi
JUMLA ya vijana 83 wanaoishi katika mazingira hatarishi wamenufaika na mradi wa kuwezeshwa kiuchumi kupitia mpango wa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi, unaotekelezwa na Shirika la Plan International ukiwa na lengo la kudhibiti mimba na ndoa za utotoni.
Mratibu wa mradi wa kuzuia mimba za utotoni wilayani Nkasi, Nestory Frank alisema jana wakati hafla ya kukabidhi vyeti na vifaa vya kazi kwa Vijana hao iliyofanyika kijiji cha Milundikwa kata ya Nkandasi wilayani humo.
Alisema kwamba katika utekelezaji wa mradi wa kuzuia mimba na ndoa za utotoni, Shirika la Plan International kwa kushirikiana na Chuo cha maendeleo ya jamii ya wananchi - Chala, wako katika mpango wa kuwafikia vijana 360 walio na umri wa miaka 18 hadi 24 ambao watawezeshwa kupata mafunzo na vifaa kupitia vikundi walivyounda.

Alisema kwa kuanzia sasa tayari wametoa mafunzo ya miezi sita kwa vijana 120, ambapo 83 wamehitimu mafunzo hayo yanayokwenda sanjari na kupatiwa vitendea kazi ambavyo ni Verehani kwa ajili ya ushonaji wa nguo kwa wahitimu wa kada hiyo na vifaa vya umeme kwa wale waliosomea fani ya umeme.
Alisema mafunzo hayo yatakuwa chachu ya wao kuondokana na umasikini wa kipato, ambao huwafanya wajiingize katika vitendo vya mahusiano ya kimapenzi wakiwa katika umri mdogo na kupata mimba zisizo tarajiwa pia kuolewa hivyo kukatishwa ndoto zao za kimaisha.
Naye, Katibu tawala wa wilaya ya Nkasi, Festo Chonya akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Said Mtanda aliagiza uongozi wa halmashauri ya Nkasi kuanza kutoa fedha kiasi Sh Milioni 138 zinazotengwa kwa ajili vikundi vya wanawake na vijana.
Alisema fedha hizo zikianza kutolewa itasaidia kuwakopesha vijana hao ambao wamehitimu mafunzo hayo ya ujasiriamali hivyo wataweza kufikia malengo yao ya kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato unaowafanya kuwa tegemezi.
"Sisi kama Serikali lazima tuunge mkono jitihada za wadau wetu wa maendeleo, kwa kuwa wao wamewawezesha kielimu,..... ni wajibu wetu kuhakikisha ile fedha inayotengwa kusaidia makundi ya vijana na wanawake inatoka kwa wakati na inatolewa kwa vikundi husika" alisema Chonya.
Pia alieleza kusikitishwa kwake na kitendo cha baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kuwasimamia vijana wao wapatao 38 ambao walishindwa kuendelea na mafunzo hayo kwamba sababu ya utoro.
Chonya alisema hali hiyo haipaswi kufumbiwa macho hivyo alitaka wazazi hao kubadilika kifikra na kuachana na mitizamo hasi kuhusu elimu hali ambayo itakuwa chachu ya kupata mafanikio ya kimaisha.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Paulina Kasunga alisema kuwa mafunzo hayo yatamsaidia sana kujipatia kipato cha kumwezesha kumudu mahitaji mbalimbali ya kifamilia hivyo kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment