Sumbawanga
KUTOKANA na halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kutokuwa na hospitali ya wilaya ni miongoni mwa sababu zinazochangia huduma za afya kutokuwa bora wilayani humo.
Mkuu wa wilaya hiyo Dk Khalfan Haule aliyasema hayo jana wakati akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili.
Alisema kuwa wilaya hiyo iliyoanzishwa mwaka 1984 mpaka leo haina hospitali ya wilaya hali inayosababisha baadhi ya huduma za afya kukosekana na kusababisha vifo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakipewa rufaa kwenda Sumbawanga mjini ambapo ni gharama na inawawia vigumu baadhi ya wananchi.
Alisema wilaya hiyo inampango wa kujenga hospitali yake ya wilaya na iwapo ikifanikiwa itasaidia kuondoa usumbufu kwa wananchi ambao wanatumia gharama kubwa kutafuta matibabu.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri hiyo John Msemakweli alisema kuwa halmashauri hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,871 na idadi ya wakazi300,549 inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo vifo vya wakina mama wajawazito.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka jana jumla wanawake 256 walijifungulia kwa wakunga kutokana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu sambamba na ukosefu wa elimu wa kutosha.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa pia sekta ya elimu hususani shule za msingi zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 1620 na halmashauri inamkakati wa kujenga vyu mbavya madarasa vitatu kila mwaka.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa huo Wangabo Aliwaagiza watendaji wa halmashauri hiyo kuongeza kasi katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.
Alisema kuwa kwa mkakati huo wa kujenga vyumba vitatu kwa mwaka itahitaji miaka14 kumaliza changamoto hiyo hali ambayo kasi hiyo ya ujenzi wa madarasa haitoshi.
Wangabo alisema tatizo la uharibifu wa mazingira ni kubwa wahakikishe wafugaji wanapewa elimu ili waache tabia ya kuzurula na mifugo nakuipunguza,kama hataki basi aondoke kwani serikali ya mkoa haita mvumilia kwakua kuna tishio la kutoweka kwa ziwa Rukwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment