Wednesday, 1 November 2017

Auawa na wasiojulikana

Na Gurian Adolf
Nkasi
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Telestina Silanda (45)  mkazi wa kijiji cha China kata ya Kate wilayani Nkasi ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana akiwa amelala nyumbani kwake.
Akizungumzia tukio hilo Charles Silanda ambaye marehemu alikuwa Shangazi yake alisema kuwa tukio  hilo lilitokea jana  majira ya saa 2 usiku ambapo watu hao wasiojulikana walipovamia nyumba ya shangazi yake na kuanza kumshambulia kwa mapanga hadi kumuua.
Alisema kuwa hadi wao wanajulishwa tukio hilo na kukimbilia eneo la tukio hilo walikuta shangazi yake akiwa ameuawa na wauaji hao na kisha kutoweka kukimbilia kusikojulikana.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho Konrad Kauzeni alisema kuwa mwanamke huyo ameuawa kinyama ambapo alikatwa miguu yake yote miwili na kuitenganisha na kiuno,kisha kuchinjwa koromeo karibu kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Alisema kuwa hadi mauaji hayo yanatokea mume wa mwanamke huyo alikuwa amekwenda porini kurina asari kwenye mizinga yake na aliporejea nyumbani alikuta mkewe kisha uwawa na waliofanya tukio hilo bado hawajafahamika.
Kwaupande wake mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda akizungumzia tukio hilo alisema serikali ya wilaya itakwenda katika kijiji hicho kupiga kura za maoni ili kuwabaini wauaji hao kwanivi tendo vya mauaji vimekuwa vikifanyika wilayani humo kwa kisingizio cha imani za kishirikina. 
"serikali ya wilaya itakwenda kijijini hapo kupiga kura ya siri ili kuwabaini wauaji kwani wapo watu wanao ua binadamu wenzao kwa kisingizio cha uchawi hatutaweza kuvumilia kuacha hali hiii endelee hivi hivi" alisema
Alisema kuwa ni jambo lisilokubalika kuona kuwa  kuna watu wanaweza kufanya uhalifu mkubwa kiasi hicho na wakaachwa ni kuwa kura za maoni zitasaidia kuweza kuwanasa wauaji hao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa wakazi wa kijiji hicho kwenda ofisini kwake kutoa taarifa za siri kwa wale wanaowafahamu waliotekeleza mauaji hayo na kuwa serikali itawalinda watoa taarifa wote.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa polisi wanaendelea na msako ili kuwabaini waliofanya mauaji hayo. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment