Saturday, 21 October 2017

Waterleeds watoa msaada

Na Walter Mguluchuma
Katavi
Shirika la Waterleeds  Program  Tanzani  WRP( T) limetoa msaada wa  gari moja kwa  Manispaa ya  Mpanda na pikipiki 26 kwa Halmashauri za mkoa wa  Katavi wenye  thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 267  kwa ajiri ya  shughuli za  mradi wa kutdhibiti  Ukimwi mkoani Katavi.
Msaada huo ulikabidhiwa jana  na mkuu wa mkoa wa Katavi Meja  Gegerali Mstaafu  Raphael Muhuga kwa  halmashauuri zote  tano za mkoa wa Katavi  katika hafla  iliyofanyika  katika viwanja vya  ofisi ya mkuu wa  mkoa huo.
Akitoa taarifa ya  msaada huo afisa mradi huo (WRP) T mkoa wa  Katavi  Dkt Baraka Mgiriwa alisema  msaada huo wa  gari  moja na pikipiki 26 umegharimu  kiasi cha shilingi milioni 268
Alisema kuwa  katika  msaada huo  Manispaa ya Mpanda wamepata   gari moja  aina ya  Picup  Land  Cruiser lenye  thamani ya shilingi milioni 168,987.707 pikipiki 4 aina ya  Honda, Halmashauri ya Mpanda imepata pikipiki 5, halmashauri ya Mlele  pikipiki 5, halmashauri ya Nsimbo pikipiki 6, halmashauri ya Mpimbwe pikipiki 5 na   ofisi ya  Mganga Mkuu wa  Mkoa  ilipata pikipiki  moja zikiwa  na  thamani ya shilingi milioni 98,800,000.
Kwaupande wake mganga mkuu  wa mkoa huo  wa Katavi  Dkt Yahaya  Huseein alisema kuwa  baada ya halmashauri hizo kukabidhiwa misaada hiyo  wanamatarajio makubwa ya kutoa  huduma  mbalimbali  katika  maeneo ya halmashauri hizo.
Alizitaja baadhi ya huduma  hizo kuwa ni kuimarika  kwa  shughuli  za usafirishaji wa  sampuli za damu kavu za watoto waliozaliwa na wakinamama wenye  maambukizi ya VVU  kwaajiri  ya kupimwa  hali ya maambukizi ya watoto wao .
Pia alisema kazi nyingine ni kupunguza uharibifu wa sampuli  za  damu  kwa watoto  waliozaliwa  na mama  wenye VVU   pamoja  na zile za kupima  wingi  wa kiwango  cha vvu  katika  damu  kwa WAVIU  wote  kwani kabla ya msaada huo walikua wakichelewa  kusafirishwa vipimo kwenda katika  maabara.
Mganga mkuu huyo  alitaja matarajio megine  kuwa ni  kuongeza  uchukuaji na usafirishaji  wa  sampuli za damu  kwa  ajiri ya  kupima  wingi wa  VVU  katika  damu  kwa  WAVIU  ili kupata tiba  sahihi  kwa wale  watakao kuwa  na idadi  kubwa  ya  kiwango  cha vvu  katika damu zao.
Pia  wanatarajia  kutekeleza  shughuli zote zilizo inishwa  katika mpango kazi kwa  wakati na kwa haraka  kwa kutumia  vitendea  kazi  hivyo  walivyo  kabidhiwa  na (WRP)T.
Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi Raphael  Muhuga alisema kuwa  msaada huo utasaidia  kuboresha  utendaji kazi kwa wagonjwa  kupatiwa huduma kwa wakati tofauti  na ilivyokua  hapo  awali.
Alizisisitiza  halmashauri  zote za mkoa huo zione  umuhimu wa   kuvitunza  vitendea kazi hivyo na wavitumie kwa makusudi yaliokusudiwa na si tofauti.
Naye mkurugenzi wa  Halmashauri ya  wilayani  yaMpimbwe  Erasto  Kiwale  alisema  kuwa   kutoka na jografia ya halmashauri  yake  pikikpiki   hizo  zitawasaidia  watumishi wa  afya kwenda kutoa huduma kwenye maeneo ambayo  hayafikiki kwa  gari kwa urahisi.
Kwaupande wake diwani wa  Kata ya  Makanyagio Haidari Sumry alisema  kuwa  mapambano ya  Ukimwi sio jambo dogo  hivyo  vitendea kazi hivyo hivyo vitasaidia  wagonjwa wengi kupata huduma kwa muda mfupi tofauti na hapo awali.
Mwisho

No comments:

Post a Comment