Tuesday, 31 October 2017

Wamiliki wa migodi Washauriwa kubadirika

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
BAADHI ya wachimbaji wadogo katika migodi ya dhahabu iliyopo mkoani Katavi wameshauriwa kubadilika kifikra na kuachana na imani potofu nakuwaona Wanawake wana laana kwani zimekuwa zikichangia kuwakosesha fursa ya kujipatia kipato kupitia uchimbaji wa madini. 

Ushauri huo ulitolewa jana na mmoja wa wachimbaji wadogo kutoka kampuni ya Sambaru Mining Group uliopo katika eneo la Chemichem Ibindi mkoani humo, Hussein Shaaban wakati akichangia katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa naTasisi ya uhifadhiwa mazingira ya(Kaeso) Kaengesa Environnant Socity Organisation iliofanyika katika ukumbi wa Libory Centre mjini Sumbawanga. 

Katika warsha hiyo iliyozikutanisha tasisi mbalimbali pamoja na wanahabari wa mikoa ya Rukwa na Katavi baadhi ya washiriki walizungumzia baadhi ya mila potofu ambazozi mekuwa zikiwasababisha wanawake wabaguliwe nakushindwa kujihusisha katika kazi za kuchimba madini.

Shaaban alisema kuwa wanawake wamekuwa wakitengwa katika shughuli za kuchimba madini kutokana na imani kuwa iwapo wakishiriki watasababisha mikosi katika machimbo hayo na hivyo kutowaruhusu kabisa kufika kufika maeneo ya machimbo. 

Alisema wapo baadhi ya wamiliki wa migodi ambao baadhi yao ni wasomi na wengine niwanasiasa wenyeuelewa lakini hawapo tayari kuona wanawake wanafika wala kufanya kazi katika migodi yao wakiamini kuwa watasababisha mikosi.

"zipo imani nyingi ambazo hazina ukweli ikiwemo kutoruhusu Wanawake kufika eneo la machimbo ya dhabhabu kwani wanaamini wana laana inayosababisha kukosa dhahabu,kupeleka vyungu vyeusi katika eneo la migodi kwani wanaamini kuwahawatapata dhahabu na hivyo kuwanyima fursa wanawake kupata kipato kutokana na uchimbaji wamadini" alisema.

Awali mkufunzi wa warsha hiyo Grace Shio ambaye ni afisaufuatiliaji nathathimini kutoka tasisi ya Kaeso alisema kuwa lengo nikuzijengea uwezo tasisi na makundi mbambali iliziweze kuelimisha jamii katika suala zima la uhifadhi wa mazingira.

Alisema kadiri maendeleo yanavyozidi ndivyo uharibifu wa mazingira unavyo ongezeka na hivyo unahitajika mkakati katika kutunza mazingira kwaajili ya sasa na vijazazi vijavyo. 

Shio lisema mikoa ya Rukwa na Katavi hivi sasa inaonekana inavutia kwa uwekezaji,iwapo hatua za kuhifadhi mazingira zisipochukuliwa hivi sasa kunahatari ya kushuhudia mikoa hiyo ikabaki jangwa kwani kuna uvunaji mkubwa wa mbao na baadhi ya watu wakiendekeza vitendo vya kuchoma misitu.

Hata hivyo alitoa wito kwa wadau wa mazingira katika mikoa hiyo kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha mazingira yanalindwa kwani mikoa hiyo inapata mvua nyingi kutokana na kuwa na mazingira mazuri lakini siku za baadae  itakabiliwa na ukosefu wa mvua kutokana na uharibifu wa mazingira. 

Mwisho

No comments:

Post a Comment