Sumbawanga
VITUO vya afya vya serikali mkoani Rukwa vimelaumiwa kwa kushindwa fursa ya kuomba mikopo katika mfuko wa bima ya afya ya Taifa kwaajili ya kununua madawa,vitendanishi pamoja na ukarabati wa majengo badala yake vituo vya watu binafsi na madhehebu ya dini ndio wamekuwa wa kinufaika na fursa hiyo.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya mkoani humo Saimon Mbaga alisema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mfuko wa bima ya Afya mkoani humo katika kikao cha kamati ya ushauri ya maendeleo ya mkoa wa Rukwa RCC.
Alisema kuwa vituo vinavyo milikiwa na serikali mkoani humo vimekuwa havitumii fursa hiyo tofauti na vituo vinavyomilikiwa na tasisi za dini na watu binafsi kana kwamba wao hawana shida ya kuboresha huduma.
Mbaga alisema kuwa vituo vingi vinavyo milikiwa na serikali vina hali mbaya katika suala la vifaa tiba pamoja na majengo lakini kitu cha kushangaza havichangamkii fursa hiyo na kubaki havina vitendanishi na miundombinu chakavu.
Alisema ili waweze kuboresha huduma zao wanapaswa kubadilika na kuomba mikopo inayotolewa na NHIF ili waweze kuboresha huduma ili wagonjwa waweze kupata matibabu ya kisasa.
Kwaupande wake mkuu wa mkoa huo Zelote Steven aliwaasa watendaji wa mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wajiunge na mfuko wa huduma ya afya kwa jamii CFH, pamoja na mfuko wa afya ya Taifa NHIF ili waweze kupata huduma.
"ifike wakati watu waache kuomba misaada ya matibabu katika nyumba za Ibada na barabarani kwani wakijiunga na huduma za bima ya afya watakuwa wanauhakika wakupata matibabu na hawata hangaika pindi watakapo ugua"alisema.
Alisema kuwa kwa kuchangia kiasi cha shilingi 76,500 kwa watu wazima na shilingi 70,400 kwa watoto wadogo wakazi wa mkoa wa Rukwa wanaweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya yaTaifa, Kinachotakiwa wapewa elimu na kuona umuhimu wa kujiunga na huduma hizo.
Aidha alisema kuwa kwa wananchi watakaoshindwa kulipa kiasi hicho hapo juu ,pia upo mfuko wa afya ya jamii CHF ambao unahitaji kiasi cha shilingi 10,000 ni vizuri wananchi wakapewa elimu ili wajiunge na mfuko huo ili wajihakikishie matibabu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment