Na Walter Mguluchuma
Mlele
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kimemchagua Walfugang Mizengo Pinda ambae ni mdogo wake na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Peter Pinda kuwa mwenyekiti wachama hicho ambaye atakiongoza kwa miaka mitano ijayo.
Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika ukumbi wa Chama cha Msingi cha wakulima Ukonongo ulipo Inyonga Wilayani Mlele huku mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa ni Waziri mteule wa Wzira ya Maji mhandisi Izack Kamwelwe ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi .
Awali Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa uchaguzi msimamizi wa uchaguzi aliwaasa wajumbe wa mkutano huo kujiepusha na kuwachagua viongozi watakao washawishi wawachangue baada ya kuwapatia rushwa.
Akitangaza matokea ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Katibu mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Katavi Joseph Makumbule alisema idadi ya wajumbe waliotakiwa kupiga kura walikuwa 541 ambao walikuwa wametoka kwenye Kata 15 za wilaya hiyo lakini waliohudhuria ni wajumbe 477.
Makumbule alifafanua kuwa wagombea walikuwa watatu kwenye nafasi ya mwenyekiti ambapo kura zilizopigwa zilikuwa 477 ambapo kura moja iliharibika na matokeo yalikuwa ni Gerald Kasela alipata kura 146 John Mbogo kura 110 na Walfugang Mizengo Pinda kura 220.
Kwa mujibu wa Kanuni mshindi wa nafasi hiyo lazima avuke nusu ya kura na hapo awali hakuna mgombea aliyefanikiwa kuvuka nusu ya kura zote hivyo ikawalazimu wajumbe wa mkutano huo wapige kura kwa mara ya pili kwa wagombea wawili walipata kura za juu ambao ni Gerald Kasela na Walfugang Mizengo Pinda.
Ambapo katika uchaguzi huo wa marudio kura 450 zilipigwa ambapo Gerald Kasela alipata kura 156 huku Walfugang Mizengo Pinda alipata kura 280 na kura 8 ziliharibika hivyo msimamizi wa uchaguzi Joseph Makumbule alimtangaza Walfugang Mizengo Pinda kuwa ndio mshindi wa nafasi hiyo na alimtangaza rasmi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mlele.
Pia mkutano huo ulimchagua Renatus Kamaninja kuwa Katibu Mwenezi wa Wilaya baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu na Mkuu wa wilaya hiyo Rachael Kasanda alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa baada ya kuwashinda wagombea tisa katika nafasi hiyo.
Kwapande wa wilaya ya Mpanda , Abal Hamis Kimanzi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo baada ya kuwashinda Method Mtepa na Wense Kaputa waliogombea nafasi hiyo katika mkutano wa uchaguzi uliofanyika kwenye uwanja wa Mpira wa Azimio Mjini humo.
Nafasi ya Katibu Mwenezi wilayaniya Mpanda alichaguliwa Elias Milwano ambaye aliwashinda wagombea wawili waliokuwa wameomba nafasi hiyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment