Sumbawanga
Wananchi mkoani Rukwa wametakiwa kuwekeza fedha zao katika mabenki mbalimbali ikiwemo benki ya Nmb ili wawe na nidhamu katika matumizi ya fedha zao sambamba na usalama wafedha hizo.
Mkuu wa mkoa huo Zelote Steven alitoa wito huo jana katika kijiji cha Mfinga wilayani Sumbawanga wakati akikabidhi misaada iliyotolewa na benki ya Nmb ambayo ni Vitanda vya wagonjwa, magodoro kwa zahanati 3 zilizopo katika wilaya ya hiyo,computer 7 kwajili ya chanji Sekondari iliyopo mjini Sumbawanga na mabati 200 kwaajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika shule ya msingi Mfinga ambavyo vyote vina thamani ya shilingi milioni 20.
Alisema kuwa ili mwananchi awe na uhakika na fedha zake ikiwemo pamoja na nidhamu ya matumizi nilazima waziweke katika mabenki ambayo yanawajali wananchi na yanarejesha faidi kwao.
Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya baadhi ya wazazi ambao wanatabia ya kuwakataza watoto wao wasifanye vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu ili wafeli kwa madai Kuwa hawanauwezo wa kuwasomesha.
"Ole wake abainike mzazi yeyote katika mkoa wangu ambaye anamwambia mtoto wake afanye vibaya katika mitihani kwa madai kuwa hana uwezo wa kumsomesha serikali itakula naye sahani moja"alisema.
Kwaupande wake mkurugenzi wa wateja wakubwa wa Benki ya Nmb nchini Richard Makungwa alisema Kuwa benki hiyo huwa inautaratibu wa kutoa faida ya asilimia 1 kila mwaka kwa jamii hivyo basi Benki hiyo imetumia sehemu hiyo kutoa katika wilaya ya Sumbawanga katika kijiji cha Mfinga.
Alisema kwakua yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Mfinga pia aliahidi kutoa mifuko 200 ya sementi ambapo 100 itaelekezwa katika ujenzi wa kituo cha polisi,na 100 katika ujenzi wa zahanati kijijini hapo.
Pia chama cha mapinduzi CCM mkoani humo ambacho kiliwakiliswa na katibu mwenezi Clemence Bakuli kiliahidi kutoa mifuko 50 ya cement, kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo John Kiondo aliahidi mifuko 50 kwaniaba ya halmashauri na mkuu wa mkoa aliahidi kutoa mifuko 100 ili kusaidia ujenzi waZahanati na Kituocha polisi huku wananchi wao wakiahidi nguvu kazi.
Mmoja wa wanawake wa kijiji hicho Teresiana Songaleli aliishukuru Benki ya Nmb kwa Msada huo kwani utasaidia wakinamama ambao walikuwa wakijifungulia chini kutokana na ukosefu wavitanda kwaajili yaz ahanati zikizopo katika wilaya hiyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment