Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Wakulima wa tumbaku wa Chama cha msingi cha Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilalamikia bodi ya Chama hicho kwa kuwaruhusu walanguzi wa tumbaku wanaonunua tumbaku kutoka mkoa wa Tabora na kuwahusu walanguzi hao wa tumbaku mfululizo katika masoko na kuwakwamisha wanachama wa chama hicho kuuza tumbaku yao waliozalisha.
Malalamiko hayo ya wanachama wa Chama hicho cha ushirika wa wakulima wa Tumbaku yalitolewa jana na wakulima hao mbele ya wandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho zilizopo katika Mtaa wa madukani mjini humo.
Ramadhan Nassoro mmoja wa wakulima hao alisema kuwa wakulima wa chama hicho wameshindwa kuuza tumbaku yao zaidi ya kilo laki tano ya msimu wa ununuzi wa tumbaku wa mwaka 2016 na 2017 kutokana na sababu mbalimbali.
Alisema sababu hizo zimesababishwa na kitendo cha bodi ya chama hicho kuwaruhusu walanguzi wa Tumbaku kuuza tumbaku yao kutoka mkoa wa Tabora na Mishamo wilaya ya Tanganyika kwenye masoko ya chama hicho hari ambayo imesababisha wakulima wa chama hicho kushindwa kuuza tumbaku kwenye chama hicho kufuatia idadi ya kilo walizokuwa wamekubaliana na Kampuni inayonunua tumbaku ya PREMIUM kukamilika.
Naye Sef Bakari alisema kuwa yeye ni miongoni mwa wakulima waliouza tumbaku yao kwenye chama hicho lakini mpaka sasa malipo yake bado haja lipwa kwa kile kinachodaiwa kuwa hawezi kulipwa malipo yao mpaka hapo kampuni ya PPEMIUM itakapo kubali kununua zaidi ya kilo laki tano zilizozidi.
Alifafanua kuwa swala la kuzidi kwa kilo za tumbaku wao wakulima haliwahusu bali wao wanachohitaji ni kulipwa kwa fedha zao tuu kwani tatizo hilo limesababishwa na viongozi wa chama hicho kushirikiana na walanguzi kwa kuwaruhusu kuuza tumbaku ya kutoka nje ya chama chao.
Aliomba Serikali ya mkoa iunde tume ya kuchunguza kwa nini kilo za tumbaku zimezidi kwa kiasi hicho kitu ambacho hakija wahi kutokea katika miaka ya uko nyuma na alishauri kwenye tume hiyo na wakulima washirikishwe.
Richard Selevesto alieleza kuwa wamekuwa wakijiuliza bila kupata majibu kwani inakuaje watu wale wale wa siku zote kila mwaka wao tuu ndio wanaongoza kwa kuuza tumbaku kila soko na mtu mmoja anauza tumbaku mpaka mitumba 600 wakati alilingani na kilimo chao na viongozi wanawaangalia tuu na swali la kujiuliza mashamba yao yako wapi waliyovuna hizo tumbaku zote .
Noelia Mbambali aldai kuwa yeye tumbaku yake inazaidi ya mwezi mmoja sasa na ipo ndani ya ghara la chama hicho lakini imeshindwa kununuliwa hadi sasa kwa kisingizio cha kutimia kwa idadi ya kilo zinazotakiwa kununuliwa na kampuni.
Kwaupande wake Osca Paulo alisema kuwa wanaimani kuwa bila walanguzi kuingiza tumbaku yao kwenye masoko yangekuwa yameisha malizika na hata malipo wangekuwa wamelipwa wakulima ndio maana tunasema walanguzi na viongozi wetu wanawahujumu wakulima wanyonge .
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Moses Shila alieleza kuwa chama chao kiliwekeana na Kampuni ya ununuzi ya tumbaku ya Premium kununua kilo 1,400,000 kwa msimu huu na tayari zimeisha timia hivyo mazungumzo yanaendelea na kampuni hiyo ili iweze kununua kilo zaidi ya laki tano zilizo zidi.
Alisema endapo kampuni kampuni hiyo haitakubali kununua kilo hizo zilizozidi upo uwezekano wa wakulima ambao wameisha uza tumbaku yao kushindwa kulipwa fedha zao kwani fedha zao zitakuwa zimeishia kwenye madeni ya pembejeo.
Alikanusha kuwa viongozi wa bodi ya chama hicho haijashirikiana na walanguzi kuingiza tumbaku ya kutoka sehemu nyingine bali ni uzalishaji tu ndio umeongezeka.
Mwisho
No comments:
Post a Comment