Monday, 25 September 2017

Wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Na Gurain Adolf
Sumbawanga. 
Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa, imewahukumu watu wawili wakazi wa kijiji cha Kaengesa wilayani Sumbawanga mkoani hapa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja na kumsababishia kifo.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jaji wa Mahakama hiyo, Dk. Adamu Mambi baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne.

Waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa ni Maurus Semwanza na Edward Chikwema ambao walimbaka Magreth Lazaro kisha kumuingizia kitu chenye ncha kali katika sehemu za siri hadi utumbo kutoka nje.

katika shauri hilo ambalo upande wa mashitaka waliongozwa na mawakili Njoloyota Mwashubila na Safi Kashindi, huku mshitakiwa akitetewa na Wakili Peter Kamyalile ambapo Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washitakiwa alitenda kosa hilo juni 10 mwaka 2012 huko katika kijiji cha Kaengesa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Ilidaiwa kuwa siku ya tukio nyakati za saa 4 usiku mwanamke huyo akiwa katika moja na baa za pombe ya kienyeji, ambapo alitoka nje kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo ndipo washitakiwa hao walipomvamia na kumziba mdomoni na matambala kisha kumpeleka kichakani ambako walimbaka kisha kumuingizia kitu chenye ncha kali ukeni na kumsababishia utumbo kutoka nje.

Ilielezwa kuwa baada ya kumfanyia ukatili huo walitokomea kusikojulikana, ndipo mwanamke huyo alipookolewa na wasamaria wema ambao walimpeleka katika Zahanati ya Kaengesa baada hospitali ya mkoa ambako alifariki dunia kutokana na kutokwa na damu nyingi katika sehemu zake za siri.

Ilidaiwa na mawakili wa serikali kwamba mtuhumiwa kabla ya kufariki aliwatambua wabakaji hao kwa majina hivyo polisi waliweza kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Awali kabla kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwashubila aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Akitoa hukumu Jaji Dk. Mambi alisema watuhumiwa wamekutwa na hatia hivyo kwa mujibu wa kifungu 196 sura 16 cha Sheria ya makosa ya jina kama ilivyofanyiwa marekebisho mwa 2002 washtakiwa wanahukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment