Tuesday, 12 September 2017

TFF ya mwaga mipira Rukwa

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
CHAMA cha Mpira wa miguu TFF imekabidhi mipira 100 kwa chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Rukwa, RUREFA kwaajili ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17.

Akikabidhi mipira hiyo mjumbe wa kamati tendaji ya TFF kanda namba 6 anayewakilisha mikoa ya Rukwa na Katavi Kenneth Pesambili alisema amekabidhi mipira hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais wa TFF Walles Kalia.

Alisema kuwa mipira hiyo imetolewa mahususi kwaajili ya Academy zinazotambulika kisheria na ni vizuri suala hilo likazingatiwa ilikuepuka malalamiko. 

Pesambili alisema Kuwa nia ya TFF ni kuona mpira unakuwa hapa nchini ndiyo maana imeamua kuwekeza kwa vijana hao ambapo watakapokuwa wataweza kuchezea vilabu vikubwa wakiwa wamefundishwa tangu wakiwa na umri mdogo. 

Alisema haihitaji muujiza ili mkoa wa Rukwa uweze kupiga hatua nilazima uwekezaji ufanyike kwa watoto lakini nilazima pia wadau washilikishwe kwani wanamchango wa hali na mali Katika kuendeleza tasnia ya soka mkoani humo.

Naye Katibu wa RUREFA Kaniki Nsokolo aliishukuru TFF na Rais wake kwa uamuzi wakutoa mipira hiyo 100 ambayo itawezesha vijana hao kucheza mpira kwakua wameipata. 

Alisema imekuwa ni mara ya kwanza kwa mkoa wa Rukwa kukabidhiwa mipira hiyo ambayo ni saizi 3.5 na saizi 4 kwa namna hiyo kwani zoezi hilo limefanyika kwa uwazi  na hakuna mizengwe na kuahidi kuwa mipira hiyo itawafikia walengwa bila tatizo.

Mmoja wa vijana wanaocheza Mpira wa miguu mjini Sumbawanga Francis Sebastian akizungumza na gazeti hili alisema kuwa kwa kitendo alichokifanya rais wa TFF kinaleta matumaini kwa wapenda soka kwani sasa mpira utapiga hatua tofauti na huko nyuma.

Naye mmiliki wa Kayombo Academy ya mjini Sumbawanga Anthon Kayombo alisema Kuwa anaimani sasa vijana mkoani watacheza Mpira kwakua TFF inania ya dhati ya kuwekeza kwenye Mpira wa watoto. 
 
Mwisho

No comments:

Post a Comment