Na Walter Mguluchuma
Katavi
WAKAZI wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi jana wamelazimika kutokula nyama ya ng'ombe baada ya kukosekana kwa huduma ya maji katika machinjio ya mji huo hali ilisababisha kuto chinjwa kwa ng'ombe katika mji huo.
Hali hiyo ilisababisha bucha za nyama Ya ng'ombe kutofunguliwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi hao na kulazimika kula kitoweo kingine tofauti na nyama ya ng'ombe
Mmojawa wauza Bucha iinayoitwa Bismilah iliyoko katika soko la Buzongwe mjini humo alisema wamelazimika kufunga bucha zao kwa siku nzima kutokana na kutokuwa na nyama ya ng'ombe ya kuuza baada ya wafanya biashara kushindwa kuchinja mifugo yao kutokana na machinjio inayomilikiwa na Manispaa ya Mpanda kukosa huduma ya maji.
Alisema siku ya jana walifika kwenye machinjio kama ambavyo huwa wanafika kwa lengo la kuchinja mifugo yao kwaajili ya kuuza nyama lakini walikuta machinjio hiyo haina huduma ya maji hali ambayo iliwalazimu kufatilia ilikujua tatizo hilo la ukosefu wa maji.
Nae mfanya biashara wa soko kuu la Manispaa ya hiyo Juma Hassan alisema kuwa tatizo la ukosefu wa maji katika machinjio hiyo limekuwa likitokea mara kwa mara na limekuwa likijirudia.
Alisema kuwa tatizo hilo huwa linatokea mara nne au tano kila mwezi na mara zote huwa wafanyabiashara wamekuwa wakipelekewa maji na uongozi wamanispaa kwa kutumia magari.
Alisema kitendo cha kushangaza jana afisa mifugo wa machinjio hiyo alikataa maji yasipelekwe kama ambavyo imekuwa maji yakipelekwa pindi machinjio hiyo inapokuwa imekosa maji .
Kwa upande wake Maneno Daniel mfanya biashara wa Bucha ya Ng'ombe katika soko la Kachoma alieleza kuwa wao wamekuwa wakilipa ushuru kwenye machinjio hayo kwa kila ng'ombe anae chinjwa ambapo wanalipa ushuru wa shilingi 5000 na kila siku wanachinjwa ng'ombe 50 sasa wao wanashangaa nikwanini maji yakosekane wakati wanalipa ushuru.
Salome John Mkazi wa Kawajense Mjini humo alisema kuwa wamelazimika kutembea kwenye masoko zaidi ya matatu kutafuta nyama hata hivyo hawakufanikiwa kupata nyama.
Kwaupande wake Meya wa Manispaa hiyo Willy Mbogo alisema tatizo hilo wahusika ni mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MUWASA ambao hawako chini ya Manispaa hiyo bali wapochini ya Wizara ya maji hivyo wao kama Manispaa wanashindwa kuwasimamia.
Mbogo lisema endapo wangekuwa chini yao hadhani kama kungekuwa na tatizo hilo linalojitokeza mara kwa mara na kuongeza kuwa pia bodi inayowasimamia MUWASA inaonekana haija kutana muda mrefu na ndio sababu watu wanafanya kazi wanavyo taka.
Mwisho
No comments:
Post a Comment