NaGurian Adolf
Sumbawanga
MWENYEKITI wa kitongoji cha Mang'o Katika kijiji cha Ntatumbila wilayani Nkasi mkoani Rukwa ameamua kuuza viwanja kwaajili ya ujenzi wa makazi kwa wakazi wa kitongozi hicho kinyume na utaratibu na kisha kuchukua fedha hizo yeye binafsi baada ya kuona halmashauri ya wilaya hiyo inachelewa kuwauzia wananchi viwanja ili wapate maeneoya kujenga nyumba.
Mwenyekiti huyo huyo wa kitongoji anayefahamika kwa jina la Jeminus Njala alikuwa akiuza viwanja hivyo kwa bei ya shilingi 50,000 nakisha kuchukua fedha hizo yeye binafsi na kuzitumia kwa matumizi yake kwamadai kuwa anaona uchungu wananchi wenzake kuhangaika sehemu ya kujenga nyumba wakati ardhi ni mali ya serikali nayeyeni kiongozi wa serikali ya kitongoji hicho.
Wakati akiendelea na zoezi hilo ndipo alipojitokeza mwenyekiti wa kijiji cha Ntatumbila kata ya Ntatumbila Logatus Kandege na kumzuia mwenyekiti wa kitongoji cha Mang’o kuuza viwanja kwa Wananchi katika eneo hilo kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mipango ya kijiji hicho.
Akizungumza mapema leo mwenyekiti huyo wa kijiji amedai kuwa alipata taarifa kuwa mwenyekiti huyo wa kitongoji alikuwa akigawa viwanja kwa watu na kutozwa shilingi 50,000 kwa kilas mmoja na kuwa alizuia zoezi hilo kuendelea na kuamuru wananchi wote waliotozwa fedha hizo kurudishiwa fedha zao
Amesema kuwa kijiji chao kupitia halmashauri ya kijiji wamepanga utaratibu mzuri juu ya viwanja hivyo na wameiomba ofisi ya ardhi ya wilaya kwenda kupima viwanja hivyo ili wajenge nyumba kwa utaratibu wa mipango miji lakini walishitushwa na taarifa za mwenyekiti huyo kugawa viwanja kwenda kinyume na maazimio ya kijiji.
Mwenyekiti huyo wa kijiji amedai kuwa mwenyekiti huyo ataitishwa kwenye kikao cha maadili ya kiiji ili aweze kuwajibishwa kwa kukiuka maazimio ya kijiji na kuwa viwanja hivyo vingweza kuleta shida na kuharibu amani ya kijiji kama zoezi hilo lingeachwa liendelee
Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Amos Mwanauta kwa upande wake amepongeza maamuzi ya mwenyekiti wa kijiji kwa kuzuia zoezi hilo kwani kijiji kina malengo mazuri na viwanja hivyo na kubwa ni kutaka viwanja hivyo vifuate mpango mzuri wa mipango miji
Diwani wa kata hiyo Richard Masai amedai kuwa mwenyekiti huyo wa kitongoji hana uwezo wa kugawa viwanja kwa watu na kuwa waliagiza kijiji kiasndae utaratibu juu ya viwanja hivyo na hajui nini kilikuwa chanzo cha yeye kukimbilia kugawa viwanja hivyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment