Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mratibu wa shirika la Marie Stopes Mkoani Katavi Seif Kajiko amelaani kitendo cha wazazi wa mtoto mwenye ulemavu wa kuongea na kusikia (bubu) ambae jina lake lim ehifadhiwa(12 ) kuozeshwa kwa nguvu na mwanaume mwenye umri wa miaka 18 ambaye naye ni bubu na hivyo kuendelea kuongeza kwa tatizo la ubakaji pamoja na mimba za utotoni mkoani humo.
Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Masigo wilaya ya Mlele Mkoani humo ambapo binti huyo ameozeshwa kwa nguvu na wazazi wake ambao walidai Kuwa hawezi kupata mtu mwingine wakumuoa isipokuwa mwanaume huyo kwakua naye ni bubu.
Mratibu wa Marie Stopes Kajiko alilaani kitendo cha mtoto huyo kuolewa kwa nguvu kwa shinikizo la wazazi wake wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kwenye uwanja wa shule ya msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda wakati wa maadhimisho ya tamasha la vijana lililowahusisha wanafunzi wa shule kumi za Sekondari za Manispaa ya Mpanda lililoandaliwa na Marie Stopes kwa kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Katavi.
Alitoa rai kwa jamii ya wananchi wa mkoa wa huo kuachaa tabia ya kuwaozesha watoto wao wa kike wakati wakiwa na umri mdogo kwani huwasababishia madhara mbali mbali ikiwemo vifo vitokanavyo na uzazi.
Alisema takwimu za mimba za utotoni zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku Mkoani Katavi na kusababisha baadhi ya wanafunzi wa kike kukatisha masomo yao kutokana na kuwa wajawazito.
Mratibu huyo wa Marie Stopes alieleza kuwa tasisi hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu kwenye shule zote za Seondari ili kuwaelimisha juu ya elimu ya uzazi wa mpango na madhara ya mimba za utotoni.
Alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na Marie Stopes katika kuk abiliana na tatizo la mimba za utotoni wamekuwa wakikabilia na na changamoto mbalimbali ikiwemo ya baadhi ya walimu wa shule za Sekondari kukataa kutoa elimu ya uzazi wa mpango isitolewe kwa wanafunzi wao.
Naya Mratibu wa vijana washirika la Marie Stopes Tanzania Daniel Mjema Emanuel alieleza kuwa lengo kuu la kongamano hilo lilikuwa ni kutoa elimu ya afya ya msingi na kuwafanya vijana watambue afya zao.
Alisema elimu hiyo ya afya ya msingi imetolewa na Marie Stopes wakati wa kongamano hilo kwa wanafunzi wa Sekondari na wasio wanafunzi ambapo pia wamefundishwa juu ya uzazi wa mpango na kujikinga na maambukizi ya VVU.
Kwa upande wake mgeni rasmi wa kongamano hilo Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Katavi Willbard Marandu alitoa wito kwa wanaume wote wa mkoa wa huo kuwa bega kwa bega katika kushirikiana na wake zao katika swala la uzazi wa mpango.
Alisema imekuwa ni tabia ya baadhi ya wanaume kuwazuia wake z ao katika swala la uzazi wa mpango kwa madai kuwa mwanamke kazi yake ni kuzaa tu.
Naye Velinancia Godwin mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mpanda alisema kuwa mimba za utotoni zimekuwa zikisababisha wanafunzi wa kike kushindwa kupata elimu waliyoitarajia .
Aliongeza Kuwa mimba za utotoni pia zimekuwa zikisababisha hasara kwa wazazi wa watoto na taifa kutopata wataalamu mbalimbali.
Mwisho
No comments:
Post a Comment