Katavi.
Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga imewahukumu watu wawili Kun yongwa hadi kufa katika kesi mbili tofauti baada ya kuwatia hatiani watuhumiwa kwa kosa la kuua kwa kusudia wake zao huku mmoj a akipatikana na hatia ya k umuua mke wake na mwingine kumuua alimuua mke wake mkubwa baada ya kumtuhumu kuwa alimuua kwa ushirikina mtoto wake kwa mke wake mdogo.
Hukumu hiyo ilitolewa na jaji wa Mahakama kuu ya Sumbawanga Jaji Adamu Mambi katika kikao cha Mahakama hiyo kilichofanyika katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Katika kesi ya kwanza Mahakama kuu ilimuhukumu Shija Sosoma(52) Mkazi wa Kijiji cha Mamba Wilaya ya Mlele kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kusudia mke wake mkubwa kwa kumchinja baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi alimuua mtoto wake wa mke mdogo kwa ushirikina.
Awali mwendesha mashitaka mwanasheria mkuu wa Mkoa wa Katavi Achiles Mulisi alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 23 mwaka 2012 huko katika Kiji ji cha Mamba.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo mshitakiwa Sosomo alimchinja mke wake mkubwa aitwaye Mwashi Nkuba baada ya kumshutumu kuwa amemuua kichawi mtoto wake wa mke mdogo.
Mwendesha mashita huyo alidai kuwa mshitakiw a baada ya kufanya mauaji ha yo alikwenda kutoa taarifa kwa balozi wa nyumba kumi na kumweleza k uwa amafanya mauaji ya kum uua mke wake mkubwa kwa kuwa amemuua mtoto wake wa mke mdogo.
Katika kesi hiyo mshitakiwa alikuwa akitetewa na mwana sheria Elias Kifunda ambap o upande huo haukuwa na shahidi yoyote zaidi ya mshitakiwa mwenyewe huku upande wa mashtaka ukiwa na mashihidi sita.
Akisoma hukumu Jaji Adamu Mambi aliiambia Mahakama k uwa kutokana na ushahidi u liotolewa Mahakamani hapo M ahakama pasipo shaka yoyote imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashita hivyo mshitakiwa amepatikana na hatia ya kifungu cha sheria na mba 196 na 197 kuua kwa kusudia
Hivyo alitoa nafasi kwa mshitakiwa ya kujitetea kabla haja som ewa hukumu hata hivyo wak ili Elias Kifunda aliielez a Mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia hiyo ambayo adhabu yake ni moja tuu kwa hiyo Mahakama itoe hu kumu kwa jinsi sheria in avyoelekeza.
Nae Mwanassheria wa Serikali Achiles Mulisi aliiomba ma hakama itoe adhabu kali kw a mshitakiwa kwani mauaji ya kuuawa kwa wanake yameshami ri sana mkoani Katavi hivyo adhabu kali ikitolewa kwa mshitakiwa huyo itakuwa ni funzo kwa watu wengine.
Jaji Adamu baada ya kusikiliza utetezi huo alisoma hukumu na kueleza kuwa mshitakiwa mahakama imemuhukumu kwa kosa la kifungu cha sheria Namba 26 a mbapo adhabu yake ni kunyon gwa hadi kufa.
Katika kesi nyingine Mahakama kuu ya Sumbawanga imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Monde Ndushi (52)Mkazi wa Kijiji cha C hamalendi Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hat ia ya kumuua mke wake kwa makusudi.
Mwendesha mashitaka mwanash eria wa Serikali Jamila Mziray aliiambia mahakama kuwa ms hitakiwa alitenda kosa hilo Machi 12 mwaka 2016.
Siku hiyo mshitakiwa alidaiwa kumuuwa mke wake aitwaye Ngole Njile kwa kumchoma na visu baada ya kukasirishwa na kitendo ch a marehemu kumnyima mahindi ndugu yake.
Mshitakiwa katika kesi hiy o alitetewa na wakili Eli as Kifunda ambapo katika utetezi wake alidai kuwa yeye hakutenda kosa hilo na siku hiyo ya tukio hakuwepo nyumbani kwake bali alikuwa amesaf iri.
Baada ya kusikliza pande hizo mb ili Jaji Adamu Mambi alitoa nafasi kwa u pande wa utetezi kuweza kujitete a kabla ya kusomwa kwa hukumu ambapo wakili E lias aliiomba Mahakama i toe adhabu kwa mujibu wa she ria inavyo eleza kwani kos a hilo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Mwanasheria wa Serikali Ja mila Mziray aliiomba Mahakama itoe ad habu kali kwa mshitakiwa kwani kitendo alichokifanya ni cha kikatili na pia a mewasababishia watoto wa marehemu kukosa huduma z a mama yao ambazo walikuwa bado wanazihitaji.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Adamu Mambi aliiambia Mahakama k uwa mshitakiwa amepatikana na hatia ya kosa la kifungu cha s heria namba 196 na 197 hivyo mahakama imem uhukumu Monde Ndusha kuny ongwa hadi kufa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment