Katavi
Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga imemuhukumu Yustine Robarti (32)Mkazi wa Kijiji cha Maji Moto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kunyongwa hadi kufa baada ya kapatikana na hatia ya kumuua mke wake na watoto wake wadogo wawili na kisha kuwatumbukiza ndani ya kisima cha kuchota maji kijijini hapo.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Adam Mambi katika vikao vya Mahakam kuu vinavyoendelea kufanyika katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria mkuu wa serikali wa Mkoa wa Katavi Achiles Mulisi.
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka Mwanasheria mkuu wa serikali wa mkoa wa katavi alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Mach 23 mwaka 2015 majira ya saa 7 za usiku baada ya kutokea ugomvi baina yake na mke wake wakati wakiwa wamelala chumbani na watoto wao ambao na hoa aliwaua.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Yustini alimpiga mke wake aitwaye Monica Lwiche( 25) na kisha baada ya kumuuwa alimtupia katika kisima cha maji na pia aliwauwa watoto wake wawili Eliza Robert(4)na Frank Robart(6) kwa lengo la kuvuruga ushahidi kwakuwa wakati akifanya kitendo hicho watoto wake walikuwa wakishuhudia.
Kabla ya kufanya mauaji hayo mshtakiwa alikuwa ametoa kauli za vitisho kuwa endapo mke wake atarudi nyumbani atafanya jambo litakalokuwa la kihistoria na ambalo halitasahaulika kwa wakazi wa kata hiyo.
Mshtakiwa katika kesi hiyo alikuwa anatetewa na wakili Patrick Mwakyusa ambapo upande huo wa utetezi ulikuwa na mashahidi wawili mshtakiwa mwenyewe na Baba yake mzazi ambapo katika utetezi huo waliiomba mahakama imwachie huru kwani upande wa mashtaka umeshindwa kudhibitisha kama kweli alitenda kosa hilo.
Pia upande huo wa utetezi ulidai kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kudhibitisha kuwa wakati anafanya mauaji hayo kuna mtu yoyote aliyeshuhudia tendo hilo la kumuuwa mke na watoto na kuwatupia katika kisima cha maji.
Utetezi huo ulipingwa vikali na mwanasheria wa serikali Achiles Mulisi kwa kile alichodai kuwa wakatika ugomvi huo unatokea mwanzoni mama mwenye nyumba alikokuwa amepanga mshtakiwa alishuhudia ugomvi huo na ushahidi wa maneno ya vitisho aliyoyatoa mshtakiwa ni ushahidi tosha kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo na kitendo cha kuwaua watoto wake wawili wanaojua kuongea na kumwacha mdogo aliyeokotwa barabarani ni ushahidi tosha.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Adam Mambi aliiambia mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na utetezi Mahakama lazima iangalie mambo matatu ambayo ni ushahidi wa mazingira,je upande wa mashtaka unadhibitisha na kama kweli mshtakiwa amehusika katika mauaji hayo au la.
Hivyo aliieleza mahamakama kuwa kutokana na maswali hayo matatu ambayo mahakama ilihoji iliridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hivyo kumtia hatiani mshtakiwa Yustin Robert kwa kosa la kifungu cha sheria namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu na alitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kabla ya kusoma hukumu.
Wakili wa mshatakiwa Patrick Mwakyusa aliiambia mahakama kutona na mshtakiwa kupatikana na kosa chini ya kifungu hicho cha sheria ambayo adhabu yake nimoja tu hana kitu chochote cha kuiomba mahakama.
Naye Mwasheria wa serikali aliiomba mahakama itoe adhabu kali li iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na hasa wanaowauwa watu wasikuwa na hatia na kutokana na mauaji kuwa mengi mkoani katavi hasa kwa wanawake ni vyema mahakama ikatoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo.
Baada ya maelezo hayo Jaji Adam Mambi alisoma kuhumu na kuieleza mahakama kuwa mshtakiwa Yustini amepatikana na hatia ya kuua watu watatu hivyo Mahakam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment