Tuesday, 25 July 2017

Mbunge kutoa vitanda vitano vya kujifungulia wakina mama wajazazito

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MBUNGE wa jimbo la Sumbawanga mjini Aesh Hilalry ameahidi kukabidhi vitanda vitano maalumu kwaajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito pamoja na magodoro 10 kwaajili ya  kituo cha afya cha Mazwi mjini Sumbawanga. 

Akihutubia katika mkutano wa hadhara katika kata ya Mazwi alisema kuwa atatoa vitanda hivyo vyenye thamani ya shilingi 180,000 lengo ikiwa ni kuboresha huduma katika kituo cha afya cha Mazwi ili wakina mama wajawazito waanze kujifufungulia katika kituo hicho. 
Alisema kuwa wakinamama wa kata hiyo bado wanategemea hospitali ya mkoa ya Sumbawanga ambayo ndiyo hospitali ya rufaa kwa mkoa wa Rukwa kwakua idara ya afya imeamua kuboresha kituo cha afya cha Mazwi ili kianze kutoa huduma mbalimbali ikiwemo ni pamoja na za uzazi, hivyo ameamua kutoa vitanda hivyo na magodoro hayo yatakayo changia kuboresha huduma 
Mbunge huyo alisema kuwa kata hiyo inawatu wengi ni vizuri kuboresha kituo cha afya kilichopo kata hiyo ili huduma mbalimbali zipatikane hapo,lengo likiwa ni kuwaondolea usumbufu wananchi wa kata hiyo. 
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo watendaji wa kituo hicho hawanabudi kujituma na kufanya kazi kwa weledi mkubwa na huruma kwa wagonjwa ili waone kuwa eneo hilo ni salama kwao na hivyo wapende kutumia kituo hicho. 
Aidha alitoa wito kwa wananchi wa kata hiyo kupata huduma katika kituo hicho kwani halmashauri imejipanga kukiboresha ili kiwe kinatoa huduma za kisasa na waache kukimbilia katika hospitali ya mkoa hali ambayo itapunguza mlundikano wa wagonjwa. 
Awali kabla ya kuhutubia mkutano huo wananchi wa Kata hiyo walimueleza mbunge wao kero mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kuwa ni pamoja na kuzuiliwa kulima bustani kando ya mto Lwiche ambapo wamekuwa wakilima bustani kwa miaka mingi. 
Mmoja wa wakazi wa Kata hiyo Maria Kasamya alimshukuru mbunge huyo kwa kuahidi kutoa vitanda hivyo ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uzazi kwa wakina mama na kumuomba awe anafanya ziara za mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo wananchi wanapata fursa ya kumweleza kero zao nae anawajibu wa kuwatatulia kwani walimchagua awe msaada kwao. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment