Friday, 7 July 2017

Mbaroni kwa kuficha watoto

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
JESHI la polisi mkoani Rukwa linamshikilia Mesha Hamad(51) mkazi wa Chanji katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo kwa tuhuma za kuwaficha watoto nane katika nyumba anayoishi kwa madai kuwa akiwafundisha dini ya Kiislamu
Tukio hilo likitokea Julai 03  majira ya saa 10 za jioni baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kuwa kuna nyumba ipo Maeneo ya Chanji kata ya Chanji tarafa ya Lwiche, Manispaa ya Sumbawanga kuwa kunawatoto wameibwa kutoka maeneo tofauti katika mkoa huo na kisha kufichwa katika nyumba ya mtuhumiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando aliwaambia waandishi wa habari Jana kuwa polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna watoto wameletwa toka Kijiji cha Namansi wilaya ya Nkasi wanaishi ndani ya nyumba hiyo kwa kisingizio cha kufundishwa dini ya Kiislamu na wamekuwa wakifungiwa tu ndani bila kutoka nje.
Baada ya taarifa hiyo askari  walifika  katika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane wakiwa na watoto nane ambapo katika mahojiano wamekiri kuwa na watoto hao na kwamba walikuwa wanawapatia mafunzo ya kidini.
Alisema kuwa Watoto  walikutwa kwenye nyumba hiyo katika mazingira ambayo siyo ya kawaida kwani ni  wadogo na wanawategemea wazazi wao na kwamba walikuwa wakilala chini ndani ya chumba kimoja kikiwa na magodoro matatu ambayo haya kuwa yakitosha kutokana na idadi hiyo ya watoto.
Watuhumiwa waliokamatwa kwenye nyumba hiyo wapo wanane ambao ndiyo walikuwa wanawafundishwa watoto hao mafundisho ya dini ya kiislamu mchana na usiku ambapo kati ya hao watoto 
Baada ya taarifa hiyo askari  walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanane wakiwa na watoto nane ambapo katika mahojiano wamekiri kuwa na watoto hao na kwamba walikuwa wanawapatia mafunzo ya kidini.
Watoto  waliokutwa kwenye nyumba hiyo katika mazingira ambayo siyo ya kawaida kwani ni  wadogo ambao bado ni wategemezi wa wazazi wao na kwamba walikuwa wakilala chini ndani ya chumba kimoja kikiwa na magodoro matatu.
Watuhumiwa waliokamatwa kwenye nyumba hiyo ni wanane ambao ndiyo walikuwa wanawafundishwa watoto hao mafundisho ya dini ya kiislam mchana na usiku ambapo kati yao watoto wa kike ni watatu na wakiume ni watano.
 Pia kati ya watuhumiwa hao mmoja kati yao alilkuwa ni mgeni kutoka Zanzibar ambaye alikuwa katika eneo la  Chanji naye pia akiwafundisha watoto hao pia.
Aidha watuhumiwa  hao  mmoja alikuwa na mpango wa kuwasafirisha watoto hao waliochukuliwa kutoka katika kijiji cha Namansi Wiliyani Nkasi Mkoani Rukwa na kuwapeleka maeneo mbalimbali ya nchi kama Dar es salaam, Dodoma na Arusha.
Kamanda Kyando aliwataja  watoto walikutwa wamefungiwa katika nyumba hiyo kuwa ni Abubakar Walala(15) mwanafunzi wa darasa la sita,Fadhil Ally(11)Mgoma, Islam, Mwanafunzi wa darasa la tatu,Bakari Mwakipesile(6), mwanafunzi wadarasa la kwanza,Said Walala(8) mwanafunzi wa darasa la kwanza. 
Wengine ni Maftah Omary(8) mwanafunzi wa darasa la  pili Juma Ally(4) ambaye ni mkazi wa Namansi na sio mwanafunzi, Kabea Issa(8)mkazi wa Namansi na hasomi shule pamoja na Hemed Uled(13) mwanafunzi wa darasa la tano na kuongeza kua watoto wote wanaosoma ni wanafunzi wa shule ya msingi Namansi,wilayani Nkasi.
Aidha katika tukio hilo Mtoto Bakari MBARUKU Mwakipesile aliweza kutambuliwa siku hiyo na mama yake mdogo aitwaye Elisia Robisoni ambaye alikuwepo eneo la tukio wakati watoto wanapandishwa kwenye gari na alidai kuwa mtoto huyo ana taarifa naye kuwa ni wiki ya tatu sasa toka amepotea kwa mama yake mzazi na walikuwa wanamtafuta na mwingine ni Fedha Sudi(15) ambaye alikuwa hasomi ni Mkazi wa kijiji cha Namansi alikutwa akiwa nyumbani kwa mtuhumiwa Mesha Hamad akiwa kama dada wa kazi katika nyumba hiyo.
Baada ya kuwafanyia upekuzi katika nyumba hiyo ili kuweza kupata nyaraka au vitu vyovyote vinavyohusiana na tukio hilo lakini kilichopatikana ni fomu nane tu ndizo zilizopatikana zikiwa na kichwa cha Habari “JUMUIYA YA ZAWIYATUL QADIRIYA TANZANIA” ambazo zilikuwa bado hazijajazwa, Fomu hizi ni fomu ya kuomba kujiunga na Madrasa kwa wanafunzi ambao wamepatikana.
Watuhumiwa wamekamatwa na upelelezi unaendelea na watafikishwa mahakamani kujibu shauri la kusafirisha binadamu kinyume na sheria za nchi.

Aidha anatoa onyo kali kwa wananchi wote wenye nia au mawazo ya kukusanya watoto wa watu bila kutoa taarifa katika vituo vya Polisi na kwa viongozi wengine wa ngazi ya kijiji na wilaya sna wakubali kukaguliwa kuhusu utendaji wao.
Pia anawataka wazazi wawe makini na watoto wao kwani siyo kila anayedai kutaka kumchumkua mwanao na kumsaidia anafanya hivyo wengine ni waongo wanawafanyia watoto vitendo kwa kiunyanayasaji wa kijinsia na kuwakosesha watoto haki za msingi kama kupata elimu.
 ni watatu na wanaume ni watano. Pia kati ya watuhumiwa hao mmoja alilkuwa ni mgeni kutoka Zanzibar.
Aidha katika watuhumiwa  hao nane mmoja  alikuwa na mpango wa kuwasafirisha watoto hao waliochukuliwa kutoka katika kijiji cha Namansi Wiliyani Nkasi Mkoani Rukwa na kuwapeleka maeneo mbalimbali ya nchi kama Dar es salaam, Dodoma na Arusha.
Pia upekuzi ulifanyika katika nyumba hiyo ili kuweza kupata nyaraka au vitu vyovyote vinavyohusiana na tukio hili, Lakini kilichopatikana ni fomu nane tu ndizo zilizopatikana zikiwa na kichwa cha Habari “JUMUIYA YA ZAWIYATUL QADIRIYA TANZANIA” ambazo zilikuwa bado hazijajazwa, Fomu hizi ni fomu ya kuomba kujiunga na Madrasa kwa wanafunzi ambao wamepatikana.
Watuhumiwa wamekamatwa na upelelezi unaendelea na wameshafikishwa mahakamani kujibu shauri la kusafirisha binadamu kinyume na sheria za nchi. 
Aidha kamanda Kyando amewataka wazazi wawe makini na watoto wao kwani siyo kila anayedai kutaka kumchumkua mtoto anania ya kumsaidia bali  wengine ni waongo wanawafanyia watoto vitendo kwa kiunyanyasaji wa kijinsia na kuwakosesha haki za msingi kama kupata elimu.
Mwisho

No comments:

Post a Comment