Monday, 12 June 2017

Sumbawanga wampongeza Magufuli

Na Gurian  Adolf

  • Sumbawanga

BAADHI ya wakazi wa mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa wamempongeza rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa TAnzania, John Magufuli kwa kuridhia  mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya pili iliyotoa ripoti baada ya kumaliza  Kazi yake na kuwapongeza wajumbe hao kwakuweka  uzalendo wa taifa mbele.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa mji wa Sumbawanga walisema kuwa Kazi iliyofanywa na kamati hiyo haikuwa ndogo  na niwazi ilikuwa ngumu kiasi cha kuweka maisha yao rehani.

Mmoja wa wakazi hao Flora Mwaga alisema kuwa haiitaji kuwa msomi  wa kiwango cha juu  ili kutambua  kuwa nchi yetu Mwenyezi  Mungu ameijalia nchi ya Tanzania utajiri mkubwa kwa kuwa na madini, ardhi pamoja na mito.

Alisema kuwa kwa miaka mingi  wananchi wa tanzania  wamekuwa masikini kutokana na kutokuwa na viongozi wenyenia ya kuisaidia nchi kwani wamekuwa wakiingia mikataba ambayo mingine  inashangaza kutokana na kuwa ni yakinyunyaji.

Mwaga alisema kuwa iwapo viongozi wangekuwa na nia ya kuwasaidia wananchi kamwe watanzania wasingekuwa na maisha magumu kwa kiasi cha kushindwa hata kumudu milo  mitatu sambamba na kukosa huduma za afya za uhakika.

Alisema kuwa iwapo viongozi wangetanguliza maslahi ya taifa mbele kwa kuingia mikataba ambayo inalinufaisha taifa hakika  nchi yetu ingekua ni yamfano barani Afrika.

Naye Afrancis Sebastian mkazi wa mjini Sumbawanga alisema kuwa hatua aliyochukua raisi  ni kubwa mno na inapaswa kupongeza huku akipongeza zaidi zaidi kuwawajibisha baadhi ya viongozi walioingia mikataba hiyo.

Alisema kuwa imefika  wakati hakuna kuoneana  aibu wala huruma kwa yeyote  ambaye ametajwa kuiingiza nchi katika hali hiyo kwani hakuna aliyebora zaidi ya maslahi ya taifa.

Sebastian alisema kuwa tunakila  sababu ya kumuombea rais  Magufuli kwa maamuzi anayochukua kwani yanawaumiza sana baadhi ya watu ambao hawapo tayari kuziona hatua hizo zikichukuliwa.

Alisema kuwa iwapo watanzania tusipojali kunufaika na rasilimali zetu tusidhani kuwa wageni na wawekezaji kutoka nje ndio watakao tupenda kwa kiasi cha tusaidiane katika kunufaika na rasilimali zetu.

Naye Peter Kapama mkazi wa mjini Sumbawanga alisema kuwa watanzania hatunabudi kuungana pamoja katika kuhakikisha kuwa tunanufaika na rasilimali za nchi bila kujali itikadi za kisiasa.

Alisema kuwa kinachohitajika ni utekelezaji wa mema yote ambayo serikali ya awamu ya tano inayafanya yaweze kuwasaidia wananchi ambao ni masikini na hawajanufaika na vya kutosha na rasilimali kutokana na waliopewa dhamana kushindwa kuisaidia nchi pamoja na nafasi walizopewa.

Mwisho

No comments:

Post a Comment