Tuesday, 20 June 2017

Mchimbaji mdogo afariki dunia kwa kuangukiwa na kifusi

Na Walter Mguluchuma
Katavi
MTU mmoja amekufa  papo hapo baada ya kufukiwa na  kifusi cha udongo wakati  alipokuwa akichimba  dhahabu katika machimbo ya Usumamilomo wilayani Mpanda mkoani Katavi.
  Kaimu   Kamanda wa  polisi wa  mkoa huo Benedick  Mapujilo  alisema kuwa  tukio  hilo lilitokea  jana  majira ya saa 8:30 mchana   katika   machimbo ya   madini ya  dhahabu ya Usumamilomo  katika   Tarafa ya  Nsimbo  Wilaya ya  Mpanda.
  Alisema  siku  ya tukio  mchimbaji huyo  aliingia   ndani ya  shimo refu maarufu kwa kina la fonka kwa lengo la kuchimba dhahabu  katika   shimo  lililokuwa na urefu wa zaidi ya  mita   hamsini.
Wakati   akiwa   anaendelea na  shughuli za uchimbaji  ndani ya  shimo  hilo kifusi cha  udongo kiliangukia  ndani ya  shimo na  kumfukia  mchimbaji  huyo  mdogo wa   madini.
  Alisema  wachimbaji waliokuwa  jirani na  eneo hilo  walipoona kifusi  hicho kimeangukia  ndani ya shimo  walipiga  mayowe ya kuitana   kwa  lengo la  kutoa msaada wa kumwokoa  mchimbaji  mwenzao.
Juhudi  za  kumwokoa  mtu  huyo  zilianza na  ndipo  walipoweza kuondoa  kifusi hicho  ndani ya  shimo  hata  hivyo walimkuta  mchimbaji  huyo  akiwa  amefariki  dunia  kutoka  na kufukiwa na udongo.
Mwenyekiti wa  wachimbaji wadogo wa  madini wa  Mkoa  wa  Katavi  Willy  Mbogo  amewataka   wachimbaji wadogo wa  madini ya  dhahabu kuacha  tabia ya kuchimba   madini kwenye   machishimo  marefu  kwa  mtindo wanaouita  Fonka kwani ni habari kwakua huwa ni rahisi kubomokewa na udongo.
Alisema   uchimbaji huo wa  mtindo wa  fonka unaotumiwa na  baadhi ya wachimbaji haufai kutumiwa  kwani unahatarisha  uhai wa  maisha yao kwani muda wowote kifusi huwa kinaweza kufunika  shimo linalokuwa  linachimbwa dhahabu.
Mwisho

No comments:

Post a Comment