Hakika Mungu ni mwema sana. Ametuwezesha leo kuwa na nguvu ya
kutafakari hatima ya nchi yetu ambayo inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2015 hapo Oktoba.Mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia makada
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijitokeza kuwania urais kupitia chama
hicho na tayari wameanza kuchuana kutangaza nia yao baada ya vikao vya
Kamati Kuu Taifa (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kumalizika hivi
karibuni mjini Dodoma na kutoa baraka zote kuanza rasmi kwa mchakato
huo.
Orodha ndefu ya makada walioonesha nia ya kutangaza kuwania ndani ya
chama hicho ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (Mbunge wa
Monduli) aliyetangaza nia Arusha, Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika,…
Hakika Mungu ni mwema sana. Ametuwezesha leo kuwa na nguvu ya
kutafakari hatima ya nchi yetu ambayo inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2015 hapo Oktoba.Mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia makada
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijitokeza kuwania urais kupitia chama
hicho na tayari wameanza kuchuana kutangaza nia yao baada ya vikao vya
Kamati Kuu Taifa (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kumalizika hivi
karibuni mjini Dodoma na kutoa baraka zote kuanza rasmi kwa mchakato
huo.
Orodha ndefu ya makada walioonesha nia ya kutangaza kuwania ndani ya
chama hicho ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa (Mbunge wa
Monduli) aliyetangaza nia Arusha, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Stephen Masatu Wassira (Mbunge wa Bunda) aliyetangazia nia yake Mwanza
na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Mchemba (Mbunge wa Ilamba
Magharibi) aliyetangaza nia hiyo Dodoma na ambaye hivi karibuni
alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa ili
aingie katika kinyang’anyiro hicho.
Wengine waliotangaza nia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli
(Mbunge wa Chato), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu
wa sasa, Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mbunge wa Katavi), Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (Mbunge wa Singida Magharibi),
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Taitus Kamani (Mbunge
Busega) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe (Mbunge wa Mtama) aliyetarajiwa kutangaza nia jana jimboni kwake.
Wapo pia Waziri Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya
(Mbunge wa Rungwe Mashariki), Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,
Januari Makamba (Mbunge wa Bumbuli), Mbunge wa Jimbo la Sengerema,
William Ngeleja na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Khamis Kigwangalla.
Makada wengine ni pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta (Mbunge wa
Urambo Mashariki), Balozi Bi Amina Salum Ali (Zanzibar) na Mtoto wa Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Nyererer, Makongoro Nyerere (sasa ni Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki). Hata hivyo, orodha hii inaweza kuongezeka
kwa sababu wengine walikuwa wakisubiri kipyenga kipulizwe.
Kwa upande wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wao bado mchakato
wao haujaanza kwa sababu watachuana baada ya kila chama kati ya vyama
vya Chadema, Cuf, NCCR Mageuzi na NLD kutoa wagombea wao.
Ninachowaomba watangaza nia ni kwamba wasitumie mwanya huo wa
kujitangaza kuchafua wenzao na badala yake wajenge hoja bila kupitiliza
kwa sababu kampeni rasmi zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
bado hazijaanza.
Kila mtangaza nia anatakiwa ajipange kuja kuwaeleza
Watanzania jinsi ya kuboresha maisha duni ya wananchi kwani walio wengi
ni magumu.
Watangaza nia wajipange kueleza jinsi ya kuondoa mfumuko wa bei za
bidhaa mbalimbali nchini ambao uko juu, wajipange kueleza wataisaidiaje
jamii? Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila
neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Kwa hiyo basi, watangaza nia watakaotumia majukwaa kuwachafua wenzao,
moja kwa moja watakuwa wamekwenda ‘nje ya reli’ kwa sababu sasa hivi
wananchi wanataka kiongozi ambaye ataeleza jinsi ya kuwakwamuwa
kiuchumi, kimatibabu na kielimu.
Ni jambo la msingi sasa kwa wana CCM kupima wagombea wao na
wasijazane tu kwenye mikutano ya kutangaza nia na kushangilia kishabiki
bila kupima neno kwa neno.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
No comments:
Post a Comment