Sunday, 7 June 2015

Malocha apata "ujiko" jimboni mwake.

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

Diwani wa Kata ya Kaengesa Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa,Ozem Chapita(CHADEMA) amewataka wa kazi wa kata hiyo kutoendekeza tofauti za kisiasa badala yake washirikiane na Mbunge wa jimbo la Kwella Ignas  Malocha(CCM) katika kujiletea maendeleo.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kianda wilayani Sumbawanga alisema kuwa kitu kikubwa na maendeleo hivyo basi wananchi wanapaswa kumuunga mkono Malocha kutokana na maendeleo makubwa waliyofikia.

Kabla ya kumkaribisha mbunge huyo ili awahutubie wananchi alisema kuwa mbunge Malocha amekuwa ni wakupigiwa mfano kutokana na maendeleo makubwa ambalo jimbo hilo limefikiwa kutokana na maendeleo.

Naye mbunge Malocha wakati akiwahutubia wananchi hao alisema kuwa bila kujali tofauti za kisiasa amekuwa akifanya kazi zake vizuri na diwani huyo hali iliyosababisha kufikia maendeleo makubwa.

aliwashukuru pia wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono kwani hali hiyo ilimpa nguvu ya kuwatumikia wananchi na ndiyo imekuwa siri kubwa ya mafanikio katika jimbo hilo.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment