Na Gurian Adolf
Sumbawanga
ZAIDI
ya watu 8877 wa kata za Kilangawane na Kipeta wilayani Sumbawanga
mkoani Rukwa hawatapata fursa ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao
kutokana na kutoandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura baada
ya muda kumalizika bila wao kupata nafasi hiyo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Kwella
Ignas Malocha, afisa mtemdaji wa kata ya Kipeta Joseph Ninde alisema
kuwa mpaka siku zilizotolewa na tume ya uchaguzi zinamalizika jumla ya
watu 3,776 ndiyo walioandikishwa ambapo matarajio ilikuwa ni kuandikisha
watu 8,651.
Alisema kuwa kushindikina kuandishwa kwa idadi
kubwa hiyo ya watu ni kutokana na tangu june 21 zoezi hilo
lilipoanzishwa katika kata hivyo mashine zilizokuwa zikitumika zilikuwa
mbovu na na hivyo kusababisha changamoto hiyo.
Naye kaimu
afisa mtendaji wa kata ya Kilangawane Eliasi Kamkwamba alisema katika
kata hiyo idadi ya watu ambapo walikuwa na sifa ya kuandikishwa katika
daftari hilo walikuwa 7,846 lakini ni watu 4,002 ndiyo waliyoandikishwa
na hivyo wengi wao pia huenda wakakosa haki yao hiyo ya msingi.
Kwaupande
wake mbunge wa jimbo la Kwella Ignas Malocha ameiomba tume ya taifa ya
uchaguzi NEC kuhakikisha inarudi tena ili iendelee kuandikisha watu
waliokosa fursa katika zoezi la kwanza kwani huko ndiyo kutakuwa
kuwatendea wananchi hao haki yao ya kikatiba.
Alisema kuwa
bila kuogopa gharama tume ya uchaguzi inapaswa kurudisha mashine za BVR
katika kata ambazo watu hawakujiandikisha na wajiandikishe kwani daima
wanapaswa kutambua kuwa Demokrasia inagharama zake na kitendo cha
kukwepa gharama ni kuifinyanga katiba pamoja na Demokrasia.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment