Wednesday, 27 May 2015

Bunge la Madagascar lapiga kura ya kumuuzulu Rais


 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/42a86893f51c2b181b51011f753d06dd_XL.jpg
Bunge la Madagascar limepitisha kwa kura nyingi muswada wa kutokuwa na imani na Rais Hery Rajaonarimapianina kwa madai ya kukiuka katiba na kutokuwa na uwezo kabisa wa kuongoza nchi.
Muswada huo uliopigiwa kura bungeni umekubaliwa na wabunge 121 kati ya wabunge 125 waliopiga kura na hivyo kupata kwa urahisi sana, thuluthi mbili ya kura zilizohitajika.
Sasa mahakama wa katiba itaamua iwapo uamuzi huo wa kumuuzulu rais unapaswa utekelezwe kivitendo au la.
Ubalozi wa Marekani mjini Antananarivo ulitangaza kumuunga mkono Rais wa nchi hiyo na kulitaka bunge kuzingatia maslahi ya taifa kwanza, hata hivyo msimamo wa ubalozi huo wa Marekani umedharauliwa kikamilifu na wabunge hao.

No comments:

Post a Comment