Na Gurian Adolf
Sumbawanga.
Baadhi ya wazazi katika kata ya Lusaka wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa
wamemuomba kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Chrispine
Mrwanda kupeleka ombi lao kwenye baraza la madiwani ili lipitishe kuwa
sheria ambayo itawapa uwezo walimu wa kuwacharaza viboko baadhi ya
wazazi wasiowatimizia mahitaji ya elimu watoto wao.
Ombi hilo walilitoa jana katika viwanja vya serikali ya kijiji hicho
ambapo Idara ya elimu halmashauri hiyo ilikuwa ikifanya ziara yenye
lengo kuboresha ufaulu katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni
utekelezaji wa sera ya matokeo makubwa sasa (BRN) katika halmashauri
hiyo.
Mmoja wa wazazi hao Datus Seleman alimuomba kaimu mkurugenzi huyo
kupokea ombi kutoka kwa wazazi wa kata hiyo kuliomba baraza la madiwani
kuanziasha sheria ndogo itakayo waruhusu walimu kuanza kuwachapa viboko
wazazi wote ambao hawawatimizii watoto wao mahitaji ya elimu.
Alisema kuwa wapo baadhi ya wazazi wamekuwa hawajali kuhusu watoto wao
kama wanakwenda hata shuleni ikiwa ni pamoja na kuwanunulia sare za
shule, madaftari na michango mbalimbali kitu ambacho kinapaswa kuwa ni
kosa la kisheria.
Naye bi Maria Maivune alisema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakitumia
pesa zao kwa kunywa pombe na kuoa wanawake wengi na hivyo kushindwa
kuwahudumia watoto wao.
"nadhani kama wazazi hao wangekuwa wanacharazwa viboko na walimu labda
wanaweza kubadirika kutokana na aibu ya kuchapwa huenda wakaanza
kuwajali watoto wao".....alisema.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi Mlwanda alisema kuwa halmashauri
itakachopaswa kufanya ni kuwabana wazazi hao ili waweze kutimiza wajibu
wao wakuwapa mahitaji wanafunzui hao ili malengo ya BRN yaweze
kutekelezeka katika Halmashauri hiyo.
Mwisho.
Friday, 25 July 2014
Mvuta bangi anusurika kwenda jela miaka miwili
Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MUUZA JI wa dawa za kulevya aina ya bangi , Ferdinand Makundi (40)
amenusurika kwenda jela miaka miwili jela baada kulipa
faini ya Sh 100,000- kwa kosa la kukutwa na kilo mbili za bangi.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi , mkoani Rukwa ,
Ramadhani Rugemalira alimuhukumu mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Mkole wilayani humo kutumikia miaka miwili jela au
kulipa faini ya Sh 100,000- baada ya kukiri kosa lake mbele ya
mahakama hiyo .
Hata hivyo mahakama hiyo ilimwachia mshtakiwa huyo baada ya
kulipa faini hiyo mahamani hapo .
Mshtakiwa huyo alikiri kosa lake hilo baada ya Mwendesha Mashtaka
, Mkaguzi Msaidizi , Hamimu Gwelo kumsomea jana makosa yake ya
awali .
Kwa mujibu wa Gwelo , mshtakiwa huyo ni mzoefu kwa sababu aliwahi
awali kutiwa hatiani na mahakama hiyo kwa kosa la kukutwa na
dawa ya kulevya aina ya bangi pia aliweza kulipa faini na kuachiwa
hivyo aliiomba mahakama impatie adhabu kali kwa kuwa bado
hajajifunza .
Hati za mashtaka mahakamani hapo zinaonesha kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo Mei , 14 mwaka huu saa saba mchana akiwa
nyumbani kwake kijijini Mkole .
Alipotakiwa kujitetea , mshtakiwa aliiomba mahakama hiyo impunguzie
adhabu kwa kuwa ana watoto kumi na mke wanaomtegemea .
Mwisho

Subscribe to:
Posts (Atom)