Na Gurian Adolf
Katavi
Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU Mkoani Katavi imewakamata watu wawili ambao walijifanya kuwa ni maafisa watasisi hiyo na kwenda kupokea rushwa ya shilingi 400,000 karibu na majengo ya ikilu ndogo.
Watuhimiwa hao waliofahamika kwa Majina ya Nicodemo Peter pamoja na Peter Mwaninsawa wakazi wa Mtaa wa Nsemlwa katika Manispaa ya Mpanda walijifanya maafisa wa takukuru na kutapeli fedha hizo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 asubuhi nje ya Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi iliyopo jirani na ofisi ya TAKUKURU.
Kamanda wa Takukuru wa Mkoani Katavi John Minyenya aliwaambia wandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia mtego ulio andaliwa na taasisi hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita ni maafisa wa takukuru kitengo cha uchunguzi.
Alisema kabla ya kukamatwa kwa wahumiwa hao walimpigia simu msiri wa takukuru na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa wa taasisi hiyo na wanalo jalada la uchunguzi za huhuma zinazo mkabili msiri huyo akihusishwa na rushwa.
Hivyo walimtaka awape kiasi cha shilingi 400,000 ili waweze kulifunga jalada hilo kwa kufuta tuhuma zinazomkabili msiri huyo ambaye ni afisa mtendaji wa Kijiji cha Vikonge Wilayani Tanganyika ambae walidai kuwa anatuhumiwa kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji ambapo alikamata mifugo ya wafugaji na kisha aliiachia baada ya kupokea rushwa ya kiasi shilingi 2,500,000.
Minyenya alieleza kwa kuwa msiri huyo ambae hapendi na anapinga vitendo vya rushwa alilazimika kufika kwenye ofisi ya Takukuru na kutoa taarifa juu ya maafisa hao bandia wa Takukuru.
Ndipo Takukuru walipoanza kufanya uchunguzi juu ya malalamiko hayo kutokana na takukuru kutokua na watu wenye tabia kama hiyo ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa watuhumiwa.
Alisema ndipo walipoandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao ambao walimtaka msiri huyo awapelekee fedha hizo nje ya jengo la Ikulu ndogo ya Katavi kwa kuwa ni jirani na ofisi yao ya Takukuru ili iwe rahisi wao kutoka ndani ya ofisi za Takukuru na kufika kwenye eneo la tukio.
Kufuatia makubaliano hayo ulipofika muda wa kupeleka fedha hizo kwa maafisa hao bandia alikwenda kuchukua fedha zilizokuwa na namba za takukuru na kisha kuwapelekea katika eneo walilokuwa wamekubaliana kwa ajiri ya kubabidhiana na mara walifika na kupokea fedha hizo nje ya jengo la Ikulu, ndipo walipokamatwa na Maafisa wa Takukuru wakiwa na fedha hizo.
Kamanda Minyenya alisema watuhiwa hao wanaendelea kushikiliwa na watafikishwa mahakamani ili kujibu mashita mawili ambayo ni kujifanya maafisa wa Takukuru na shitaka la pili ni kuomba na kupoke rushwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment