Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu kifungo cha maisha Lazaro Ngomalala(50)mkazi wa Kijiji cha Sibwesa wilaya ya Tanganyika baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka tisa wa shule ya msingi Sibwesa.
Akisoma hukumu hiyo jana hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa alisema mahakama imeridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashitaka uliotolewa mahakamani hapo ukiwemo wa mwanafunzi aliyebakwa.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo Hakimu Ntengwa alisema kuwa mtu yoyote anayefanya kitendo kama alichofanyiwa mtoto huyo anakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 kifungo kidodo cha kwanza na cha pili na na kifungu cha sheria namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu.
Alieleza kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka akiwemo mtoto mwenyewe aliyebaka na mtoto mwenzake ambae alishudia tukio hilo mahakama pasipo kuachashaka yoyote imemkuta na hatia mshitakiwa Ngomalala.
Hakimu Ntengwa alisema miuongoni mwa ushahidi uliosababisha mahakama imtie mstuhumia hatiani ni ushahidi uliotolewa na mtoto aliyebakwa pamoja na mtoto mwenzake mwenye umri wa miaka saba licha ya kuwa na umri mdogo walitoa ushahidi kwa ufasaha mkubwa dhidi ya tukio hilo.
Pia Mahakama ilijiridhisha na ushahidi uliotolewa na muuguzi wa Zahanati ya Sibwesa aliyemfanyia uchunguzi na kubaini mtoto huyo alikuwa amembakwa hali iliyomlazimu muuguzi huyo amwanzishie dawa ya kuzuia maambukizi ya virus vya ukimwi.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo hakimu huyo alitoa nafasi kwa mtuhumiwa kama anayosababu ya msingi ya kujitetea ili aishawishi mahakama impunguzie adhabu, ambapo aliiomba Mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa yeye hakutenda kos hilo bali amesingiziwa na mama mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimdai fedha alizomkopesha.
Baada ya utetezi huo hakimu Ntengwa alisema kuwa kutokana na mshitakiwa kupatika na hatia Chini ya kifungu cha sheria namba131 kifungu kidogo cha cha tatu kinachoeleza mtu yoyote atakae mbaka mtoto mwenye umri wa chini ya miaka kumi adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.
Hivyo kutokana na mshitakiwa Ngomalala kupatikana na kosa hilo mahakama imemuhukumu kuanzia jana kutumkia kifungo cha maisha jela.
Awali kwenye kesi hiyo Wakili wa Serikali Fravian Shiyo alidai Mahakamani hapo kuwa Lazaro alitenda kosa hilo Oktoba 12 mwaka jana majira ya saa 4 asubuhi kijijini hapo.
Ilidaiwa kuwa siku ya tukio mshitakiwa alikuta mtoto aliyemtendea kitendo hicho akiwa na mtoto mwenzake wakiwa wanacheza jirani na nyumba yao ndipo alipowadanganya wafuate nyumbani kwake ili akawape fedha wakanunue biscuit na soda.
Shiyo alieleza kuwa wakati wakiwa wanaelekea nyumbani kwa mshitakiwa walipofika kwenye eneo la tanki la maji mtuhumiwa Lazaro alianza kumbaka licha ya mtoto huyo kupiga kelele lakini hakuweza kumwachia mpaka alipo maliza aja yake .
Mwanasheria aliiambia mahakama hiyo baada ya kufanyiwa kitendo hicho mtoto huyo aliyebakwa alikwenda kutoa taarifa kwa wazazi wake huku akiwa analia na wazazi wake walitoa taarifa kwa askari mgambo wa kijiji ambaye alimkamata na kumfikisha kituo cha polisi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment