Sumbawanga
WAKAZI wa vijiji vya Kalepula A na B kata ya ulumi wilaya ya kalambo mkoani Rukwa wamelazimika kufanya sherehe kwa siku nzima baada ya kuondokana na tatizo la maji lililo dumu tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho zaidi ya miaka 20 baada ya serikali wilayani humo kuchimba kisima cha maji kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 50.
Kabla ya kuchimbwa kisima hicho wananchi hao walikuwa wanalazimika kutembea umbali wa zaidia ya kilomita tano wakitafuta maji huku wakina mama wakilazimika kuamka majira ya saa tisa za usiku kwa lengo la kutafuta maji hayo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa sherehe hiyo ya kufurahia kisaima hicho, wananchi hao wamesema ujezi wa kisima hicho umewasaidia kuondokana na tatizo la maji na kuiomba serikali kuwasambazia haraka katika nyumba zao ili wanze kuyatumia maji hayo.
Lucia Katata mkazi wa kijiji cha Kalepula A alisema kuwa wameteseka kwa muda mrefu kwa kuamka nyakati za alfajiri kwa lengo la kutafuta maji, huku wengine ndoa zao zikivunjika na baadhi kupata kipigo kutoka kwa wenzi wao walikuwa wakiwatuhumu kutumia kisingizio cha kutafuta maji na kusaliti ndoa zao.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Michael Mazila, alisema kuwa kisima hicho kilinza kuchimbwa mwaka 2015 lakini kutokana na ujenzi wa kusua sua baadhi ya watu walichukia na kuamua kukifukia kwa hasira nyakati za usiku huku wakidai kuwa mkandarasi aliyepewa zabuni ya kuchimba kisima hicho hana nia ya kuwatoa katika dhiki waliyo nayo.
Kutokana na kitendo hicho mkandarasi alianza kukifukua upya kisima hicho na kulazimika kuajiri walinzi ambao walikuwa wakilinda kwa wakati wote mradi huo ukiwa unatekelezwa.
Alisema kuwa ili kisima hicho kiwe endelevu na kitoe maji kwa muda mrefu wananchi wanaoishi karibu na kisima hicho wamepigwa marufuku kufanya shughuli za kilimo karibu na kisima hicho hivyo niwajibu wao kuheshimu utaratibu huo.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Modest Tuseko alisema kuwa mbae wananchi walikuwa wakiteseka kwa kukosa huduma ya maji safi na salama, huku wakipatwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo homa ya matumbo kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salama.
Alisema kuwa hivi sasa hatua inayofuata ni kusambaza maji katika nyumba za wakazi wa kata hiyo ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji kwani baadhi ya nyumba zipo umbali mkubwa kutoka kilipo kisima hicho.
Mwisho
No comments:
Post a Comment