Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MKUU wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Methew Sedoyeka amepiga
marufuku biashara ya kuuza pombe na vilevi vingine nyakati za asubuhi
badala yake biashara hiyo ianze kufanyika kuanzia saa 9;00 za mchana
baada ya muda wa kazi.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwakwe Methew Sedoyeka
alisema kuwa biashara hiyo imekuwa ikisababisha watu kunywa pombe
asubuhi na kushindwa kufanya kazi hali inayowasababisha washindwe
kujipatia kipato.
Alisema haiwezekani wilaya hiyo ikawa na walevi wengi kupita
wazalishaji kwa kufanya kazi na hivyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na
usalama vya wilaya kuhakikisha vinachukua hatua kwa watu watakao kaidi
amri hiyo ya DC.
Aidha alitoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga pamoja na
wilaya ya Sumbawanga kujituma katika kazi ili waweze kupata kipato
kikubwa kitakacho wawezesha kujipatia maendeleo kutokana na nguvu kazi
yao.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Sumbawanga wamepokea kwa mtazamo tofauti
agizo hilo la mkuu wa mkoa ambapo baadhi yao wamepongeza agizo hilo
huku wengine wakilalamikia kwamadai kuwa wao uzalishaji wao unatokana
na kuuza vilevi na wanalipa kodi.
Mmiliki mmoja wa baa mjini humu Peter Kayanda alisema kuwa wapo watu
kazi zao wanafanya nyakati za usiku kama walinzi na waliopo zamu za
usiku kazini muda wao wa kupumzika na kupata starehe unakuwa ni
asubuhi jioni ni muda wa kuelekea kazini.
Alisema kuwa pia serikali inapaswa kufahamu kuwa makampuni yanayouza
vilevi hapa nchini ndiyo yanaongoza kwa kulipa kodi tofauti na
makampuni ya uchimbaji wa madini hatua hiyo inaweza kusababisha
kupungua kwa mapato hata ya serikali.
Naye Monica Mayage mkazi wa Sumbawanga alisema kuwa kitendo hicho
kitasababisha pia watumishi walevi wa sekta binafsi na serikali kuwepo
kazini muda wote wa kazi na kuwajibika kwani baadhi yao wamekuwa
wakitoroka hata kazini kwajili ya kwenda kunywa pombe.
Mwisho
Tuesday, 12 April 2016
Wafugaji Mlele wamuangua DC
Na Gurian Adolf
Mlele
WAFUGAJI wilayani Mlele mkoani Katavi wamemuangukia
mkuu wa wilaya hiyo Issa Njiku wakimuomba asitishe kwanza agizo lake
la kuwataka waondoke katika mapori wanapofugia kwa madai kuwa maeneo
hayo ni mapori tengefu.
Akiongea na waandishi
wa habari jana mwenyekiti wa Chama cha wafugaji mkoa wa
Katavi (CCWT) Mussa
Kabushi alisema chama
cha wafugaji kinamwomba mkuu huyo
wa Wilaya asitishe
zoezi alilopanga lianze
kufanyika Aprili 20
katika Kata ya Ugala
la kuwahamisha wafugaji waliofuga
mifugo katika mistu ya
Kata ya Ugala katika vijiji vya
Katambike Kamili na Kitongoji
Sanda.
Alisema kutokana na agizo la mkuu huyo wa wilaya la
kuwataka wafugaji waondoke katika maeneo waliyopo hivi sasa
linawasababishia usumbufu mkubwa na kuwafanya wajihisi kana kwamba
wananyanyasika ndani ya nchi yao na wamekuwa wakifukuzwa fukuzwa hovyo
bila utaratibu kama ni wakimbizi walioko ugegenini.
Kabushi alisema kuwa katika wilaya hiyo kuna mgawanyo wa matumizi ya ardhi ambapo
eneo walilotengewa wafugaji ni Ekta
3,765 sawa na hekta 9,430 ambalo linatosha kulishia
mifugo 1,886 wakati mifugo
iliyopo ni zaidi ya elfu
kumi .
Alisema kutokana na kutokuwa na eneo la kutosha
kumesababisha wafugaji kuchungia mifugo hadi nje ya eneo walilotengewa
hatua ambayo inatafsiriwa na serikali ya wilaya kuwa wamevamia katika
maeneo ya hifadhi na hivyo kufukuzwa bila hata majadiliano.
Mwenyekiti huyo wa wafugaji alisema kuwa kwakuwa
wakati mchakato wa ugawaji maeneo hayo unafanyika wafugaji
hawakushirikishwa ni vizuri buasra za mkuu wa wilaya zikatumika na
akaitisha mkutano ili zoezi hilo lifanyike upya kwa kuwashirikisha
wafugaji ili kuondoa hata hatari ya mivutano baina ya wafugaji na
wakulima.
Hivi karibuni Kwenye mkutano
wa hadhara katika kata ya Ugalla wilayani humu,mkuu huyo wa Wilaya
aliagiza ifikapo April 20 wafugaji wote wanaochungia ng'ombe katika
hifadhi na maeneo mengine ambayo ni tengefu waondoke mara moja pia
aliwataka wafugaji hao wapunguze
mifugo yao ambapo aliwasahauri waipunguze hadi kufikia mwenye ng'ombe 200 abaki na 100 na mwenye 100 abaki na 50.
Mwisho
Serikali ya kijiji yawaonya wafugaji kutembea na silaha za jadi
Na Gurian Adolf
Nkasi.
SERIKALI ya kijiji cha Ntatumbila wilayani Nkasi Mkoani Rukwa imewapiga marufuku watu wa jamii ya wafugaji kwenda maeneo ya starehe wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mapanga hali ambayo inahatarisha usalama wa eneo husika.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Ignas Kanjele alipiga marufuku hiyo katika mkutano wa kijiji uliofanyika jana uliokuwa na lengo la kuzungumzia hali ya usalama pamoja na kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji hicho.
Alisema kuwa katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya muda mrefu kwa wafugaji kutembea wakimwa na sime, mkuki, mapanga na hata marungu hali inayosababisha hofu kwa baadhi ya wananchi kwani hawajui usalama wao wanapokutana na mtu huyo.
Mwenyekiti huyo wa ulinzi na usalama wa kijiji hicho alisema kuwa kutokana na kutembea na silaha hizo bila serikali yake kuchukua hatua baadhi yao wamekuwa wakiwapiga wananchi na hata kuwajeruhi hali ambayo haivumiliki kijijini hapo.
“ kuanzia leo hii ni marufuku kwa wafugaji kutembea na silaha za jadi kwakua hii inasababisha wawapige wananchi fimbo na kuwaumiza huku wengine wakienda katika sehemu za starehe kama harusini, mpirani wakiwa na fimbo na sime atakaye kamata atachukuliwa hatua”
Aidha aliliagiza jeshi la mgambo kijijini hapo kuhakikisha kuwa wanawasaka watakaokiuka amri hiyo ili kuondoa vitendo vya uvungaji sheria kwani hata migogoro ya wakulima na wafugaji inatokana na wengine kutembea na silaha hali inayosababisha kundi jingine litumie silaha yanapokabiriana makundi haya mawili.
Kufuatia marufuki hiyo baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakizungumza na gazeti hili waliushukuru uongozi wa kijiji hicho walidai kuwa tabia hiyo imekuwa ikiwakera kwa muda mrefu lakini walikuwa hawana namna ya kufanya.
Monica Kavishe mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa baadhi ya wafugaji hao wamekuwa wakiwachapa fimbo na kuwajeruhi na wamekuwa wakifanya ubabe kijijini hapo kwa madai kuwa wanauwezo hata wa kifedha wa kuwadhibiti viongozi wa serikali lakini kutokana na maamuzi ya mwenyekiti Kanjele inaonesha ameamua kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya rais John Magufuli.
Mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)