Na Gurian Adolf
KUTOKANA
na kuongezeka kasi ya waganga wa jadi kutumia viungo vya wanyama pori
katika kutoa tiba kumechangia kuongezeka kwa ujangili katika hifadhi ya
taifa ya Katavi iliyopo mkoani Katavi.
Baadhi ya wakazi wa
mkoa huo wamesema kuwa kitendo cha waganga wa jadi kutumia viungo vya
wanyama hao kumesababisha watu wanaopewa masharti ya kutafuta viungo
hivyo ili watibiwe kuwinda wanyama hao ili kupata vitu wanavyoagizwa na
waganga hao.
Mmoja wa wakazi Hao Fransis Kashamakula
akizungumza na nipashe alisema kuwa wakati mwingine wanapokwenda
kutibiwa kwa waganga hao wamekuwa wakiambiwa ili wapone ni sharti
wapeleke ngozi ya simba ama kwato za swala na hivyo wao kulazimika
kutafuta vitu hivyo.
Alisema kuwa niwazi hakuna namna
nyingine isipokuwa kuwinda mnyama huyo ili kupata mahitaji hayo ambapo
kitendo hicho kinachangia kuua wanyama kutokana na kuagizwa na waganga
hao wa jadi.
Alisema watu wengine ni wakulima wa tumbaku
mkoani humo ambao wanaamini kuwa waganga wa jadi hutumia viungo vya
wanyama hao kama kucha ngozi na vinginevyo kufanya zindiko katika
mashamba yao ili wakulima wenzao wasiwaibie mazao yao shambani kwa njia
za kishirikina.
Aidha imani nyingine iliyopo ni kuwa
waganga hao hutumia vitu hivyo kuzuia mvua ya mawe isinyeshe kwani mvua
hivyo inaponyesha shambani mawe huangukia majani ya tumbaku na kuchanika
chanika na hivyo kuto faa tena hivyo waganga wamekuwa wakitumia viungo
vya wanyama hao ili kufanya zindiko mvua hiyo isiharibu majani hayo ya
tumbaku.
Naye Maria Kaswaya mkazi wa mkoa huo alisema kuwa
pia kunabaadhi ya magonjwa ya watoto yanatibiwa na waganga hao kwa
kutumia ngozi na manyoya ya wanyama hivyo hulazimika kutafuta vitu
ambavyo vinaagizwa na waganga hao na hivyo kusababisha kuuawa kwa
wanyama katika hifadhi hiyo.
Desemba 27 mwaka jana, mganga wa jadi aliyefahamika kwa jina la Vitus Chomba(42)
mkazi wa Sumbawanga mjini mkoani Rukwa alishikiliwa na polisi wa wilaya
ya Mlele mkoani Katavi baada ya kukutwa na nyara za serikali ambazo
alieleze kuwa huwa anazitumia wakati wa kutibu na kuroga pindi wateja
wake wanapohitaji huduma hizo.
Mwisho
Thursday, 31 December 2015
Majangili wanaswa, waua tembo wanne
Na Gurian Adolf
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma
za kuwakamata na meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 120
ambayo ni sawa na Tembo wazima wanne .
Watuhumiwa hao watatu waliokamatwa na meno hayo ya Tembo wametajwa
kuwa ni Bathromeo Agustino(26) Geofrey Exavery(40) na Elias
Mwelela( 40) wakazi wa Mtaa wa Aitel Kata ya Uwanja wa Ndege
Manispaa ya Mpanda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia
waandishi wa Habari kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Desemba 29
majira ya saa 4 usiku katika Mtaa huo wa Airtel waliko kuwa wakiishi.
Alisema Askari Polisi na Askari wa (TANAPA) wa HIFADHI ya Taifa
ya mbuga ya Katavi walipatataarifa za siri kutoka kwa Raia wema kuwa
katika Mtaa huo kuna watu wanamiliki nyara za Serikali.
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa baada ya taarifa hizo kuwa
zimepokelewa na ufuatiliaji ulifanyika katika makazi waliokuwa
wakiishi watuhumiwa hao watatu.
Alisema ndipo siku hiyo ya tukio upekuzi ulipofanyika kwenye makazi ya
watuhumiwa na katika upekuzi huo watuhumiwa hao walikutwa na meno ya
Tembo vipande 12 vyenye thamani ya shilingi milioni 120 ambayo ni
sawa na tembo wanne hai yakiwa kwenye makazi yao.
Kidavashari aliendelea kueleza kuwa watuhumiwa mbali ya kukamatwa na
meno hayo ya Tembo pia walikutwa na mzani mmoja na Pikipiki aina ya
Sanya yenye Namba za usajiriT.552 CZE.
Alisema watuhumiwa wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa hatua za upelelezi na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi
utakapo kuwa umekamilika .
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa onyo kwa Wananchi kuacha
mara moja kujihusisha na biashara za nyara za Serikali na biashara
haramu .
Mwisho
Tuesday, 29 December 2015
Apigwa radi akienda shambani
Na Gurian Adolf
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Grace Nobert (36) mkazi wa kijiji cha
Kipundukala katika mamlaka ya mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa amekufa papo hapo baada ya
kupigwa radi.
Akizungumza na
Nipashe mume wa marehemu Anord Kaunda
alisema kuwa mauti hayo yalimkuta mkewe Desemba 27 majira ya saa 9 alasiri akiwa njiani akielekea shambani.
Alisema
tukio la kupigwa radi mkewe huyo kilitokea muda mfupi baada ya kuagana
na mke wake huyo aliyemuaga kuwa anakwenda shambani kupalilia maharage
naye mumewe alimuaga kuwa alielekea kanisani katika ibada ya jioni.
Kabla
hajafika
kanisani alipigiwa simu na mmoja wa wakazi wa kijiji hicho na kupewa
taarifa kuwa mkewe kafariki taarifa ambazo zilimsababishia mstuko
mkubwa.
Baada ya taarifa hizo alielekea eneo la tukio na kushirikiana na
majirani zake kisha walimkimbiza hospitali na walipofika madaktari
waliwaeleza kuwa mwanamke huyo alifariki dunia palepale alipopigwa na
radi.
Naye Mwenyekiti wa
kijiji hicho Kiliani tinga alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa
marehemu huyo alikutwa na majeraha kifuani na katika eneo la chini ya tumbo na
nguo zake zilichanwachanwa na mwili wake ulikuwa mweusi kupita kiasi.
Alisema kuwa
polisi walifika eneo la tukio kwalengo la kujiridhisha kuwa kifo hicho kweli kilitokana
na kupigwa radi na si vinginevyo.
Diwani wa
kata hiyo Philipo Kapembwa alisema kuwa katika maeneo hayo kumekuwepo na radi
za mara kwa mara ambapo katika siku za hivi karibuni mbuzi kadhaa walikufa baada ya kupigwa na radi.
Alisema
kumekuwepo
na minong’ono kwa majirani wa familia hiyo ya kuwapo kwa imani za
kishirikina kufuatia tukio hilo lakini wana familia wa marehemu huyo
walikataa na kuongeza kuwa kifo hicho kimetokana na mapenzi ya Mungu.
mwisho
Sangoma anaswa na Nyara za serikali
Na Gurian Adolf
MGANGA wa Jadi aliyefahamika kwa jina la Vitus Chomba(42) mkazi wa Sumbawanga mjini mkoani Rukwa anashikiliwa na polisi wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi baada ya kukutwa na nyara za serikali ambazo alieleze kuwa huwa anazitumia wakati wa kutibu na kuroga pindi wateja wake wanapohitaji huduma hizo.
Tukio la kukamatwa kwa tabibu huyo wa tiba mbadala lilitokea Desemba 27 majira ya saa 1;00 za jioni baada ya wakazi wa eneo alilokuwa akiishi kumtilia shaka kutokana na kukutana na watu kwa siri wakati yeye ni mgeni katika eneo hilo.
Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Nsekwa wilayani Mlele mkoani Katavi Amos Ngozi alisema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa wakazi wa kata hiyo wakieleza kuwa kunamtu ambaye amekuwa akikutana kwa siri kubwa na baadhi ya wakazi wa kata hiyo hali iliyosababisha hofu kwa baadhi ya wananchi.
Alisema baada ya taarifa hizo alitoa taarifa polisi ambapo kwa kushirikiana na polsi hao walivamia katika nyumba anayoishi mganga huyo na kuanza kuifanyia upekuzi na katika beji lake la nguo walikuta kuna Ngozi ya simba, maini ya Swala pamoja na ngozi ya paka pori.
Mtendaji huyo wa kata alisema kuwa vitu vingine walivyomkutanavyo ni nyama ya Sungura, kwato za pundamilia pamoja na mkia wa nyati ambapo alieleza kuwa yeye ni mganga wa jadi na huwa anatumia vitu hivyo wakati wa kutibu ama kuroga kutokana na huduma anayohitaji mteja wake.
Alisema mganga huyo alifika katika kijiji cha Inyonga wilayani humo kwalengo la kufuata wateja wake ambao walikuwa wamemuita awatibu na kuwafanyia zindiko pia kutafuta vitu ambavyo atavitumia katika kutengeneza dawa ambazo anatumia kutibia wateja wake.
Hata hivyo mtendaji Ngozi alisema mganga huyo alichukuliwa na polisi na kushikiliwa katika kituo cha polisi kutokana na kukutwa akiwa na nyara za serikali, kosa la kufanya tiba za jadi wakati hana kibali cha kufanya kazi hiyo.
mwisho.

Saturday, 26 December 2015
Noah yauwa watatu mtoni
Na Gurian Adolf
WATU watatu wamekufa
maji wakiwa wanatoka katika mahemezi ya
sikukuu ya Krismasi baada ya gari aina ya NOA walilokuwa wamepanda kutumbukia katika mto Kilambo wakati likiwa
safarini kutoka katika kijiji cha Muze wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa likielekea katika kijiji cha Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi.
Kwamujibu wa taarifa kutoka kwa Diwani wa kata ya Muze
Kalolo Joseph Ntila alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 24 majira ya saa 4;20 usiku ambapo gari hilo
likiwa na abiria saba lilipoacha njia na kutumbukia katika mto huo.
Alisema kuwa baada ya gari hilo kutumbukia mtoni baadhi ya
abiria walifanya jitihada za kujiokoa ambapo walifanikiwa kutoka huku wanawake
wawili na mtoto mdogo mmoja walishindwa kutoka ndani ya gari hilo na kufa maji
wakiwa ndani ya gari hilo.
Diwani Ntila alisema kuwa baada ya abiria hao kutoka
walijitahidi kutoa msaada kwa watu waliokuwa wamebaki ndani ya gari hilo lakini
hawakufanikiwa kutokana na maji mengi na walipofanikiwa waliwatoa wakiwa
wameshafariki dunia.
Alisema kuwa watu hao bado hawajafahamika majina yao lakini
miili ya marehemu hiyo ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika
kituo cha afya cha Muze kwaajili ya kusubiri kutambuliwa ili ndugu zao
wakafanye maziko ya watu hao.
Aidha diwani huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Sumbawanga alisema kuwa barabara katika eneo hilo si nzuri hasa
nyakati hizi za masika pindi mvua zinaponyesha kumekuwa na utelezi hali
iliyosababisha gari hilo kuteleza na kutumbukia mtoni.
Alitoa wito kwa madereva wanaofanya safari kupitia barabara
hiyo kuwa waangalifu katika nyakati hizi za masika kwani tahadhari
isipochukuliwa huenda watu wakaendelea kupoteza maisha kutokana na ubovu wa
barabara hiyo.
Mwisho.
Thursday, 24 December 2015
wananchi wajutia kuipa ardhi Serikali.
Na Gurian Adolf
SERIKALI ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi imesema kuwa imeamua kufunga safari na kwenda kumuona waziri wa Afya ili waweze kupewa uhakika wizara yake itatoa fedha lini za kuwalipa fidia wananchi waliotoa ardhi yao ili iweze kujengwa hospitali ya wilaya hiyo kwani imekuwa ni muda mrefu hivi sasa.
Mkuu wa wilaya hiyo Issa Njiku aliwaambia wananchi
wa wilaya hiyo wawe wavumilivu kwani baada ya muda mfupi watapewa majibu
ambayo yatamaliza tatizo la muda mrefu la wao kudai fedha zao za fidia
kutokana na kutoa ardhi ili ijengwe hospitali hiyo.
Alisema wananchi wamekuwa wakidai fedha zao ili waweze kulipwa na wanunue ardhi katika maeneo mengine ambapo wataweza kuendelea na shughuli za uzalishaji ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na ujenzi wa nyumba bora na za kisasa.
Njiku alisema kuwa mara kadhaa serikali ya wilaya hiyo wamekuwa wakiwasiliana na watendaji wa wizara ya afya na kupewa majibu ambayo hayawaridhishi wananchi hivyo yeye, mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na mganga mkuu wa hospitali hiyo watafunga safari kwenda wiazara ili wakaelezwe ni lini fedha hizo zitakuwa tayari.
Alisema imefika wakati wananchi wameanza kupoteza imani na viongozi hao wa wilaya inaonekana kama hawalipi uzito suala lao na wao ndiyo wanaoishi na wananchi hao na hivyo lawama zote wanazibeba wao hivyo wanajisikia vibaya.
Mmoja wa wananchi wanaodai fidia Fransis Mikidadi alisema kuwa wamechoka kuvumilia na hawaamini kuwa viongozi wao wanalifuatilia suala lao kwa umakini kwani lingekuwa limekwisha malizika kwani serikali haiwezi ikakosa fedha za kuwalipa deni lao.
Alisema wananchi hao wanaendelea kuchangishana fedha kwaajili ya naauri ili baada ya sikukuu ya mwaka mpya wafunge safari kwenda kuonana raisi John Magufuli ili aweze kuwasaidi wapatiwe fedha hizo ama ikibidi akiisoma habari hii katika gazeti la Nipashe awasaidie kwani wanateseka na wanazidi kuwa masikini kwa ujinga wa kutoa ardhi yao na kuipa serikali inayowasumbua.
mwisho
SERIKALI ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi imesema kuwa imeamua kufunga safari na kwenda kumuona waziri wa Afya ili waweze kupewa uhakika wizara yake itatoa fedha lini za kuwalipa fidia wananchi waliotoa ardhi yao ili iweze kujengwa hospitali ya wilaya hiyo kwani imekuwa ni muda mrefu hivi sasa.
Alisema wananchi wamekuwa wakidai fedha zao ili waweze kulipwa na wanunue ardhi katika maeneo mengine ambapo wataweza kuendelea na shughuli za uzalishaji ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na ujenzi wa nyumba bora na za kisasa.
Njiku alisema kuwa mara kadhaa serikali ya wilaya hiyo wamekuwa wakiwasiliana na watendaji wa wizara ya afya na kupewa majibu ambayo hayawaridhishi wananchi hivyo yeye, mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na mganga mkuu wa hospitali hiyo watafunga safari kwenda wiazara ili wakaelezwe ni lini fedha hizo zitakuwa tayari.
Alisema imefika wakati wananchi wameanza kupoteza imani na viongozi hao wa wilaya inaonekana kama hawalipi uzito suala lao na wao ndiyo wanaoishi na wananchi hao na hivyo lawama zote wanazibeba wao hivyo wanajisikia vibaya.
Mmoja wa wananchi wanaodai fidia Fransis Mikidadi alisema kuwa wamechoka kuvumilia na hawaamini kuwa viongozi wao wanalifuatilia suala lao kwa umakini kwani lingekuwa limekwisha malizika kwani serikali haiwezi ikakosa fedha za kuwalipa deni lao.
Alisema wananchi hao wanaendelea kuchangishana fedha kwaajili ya naauri ili baada ya sikukuu ya mwaka mpya wafunge safari kwenda kuonana raisi John Magufuli ili aweze kuwasaidi wapatiwe fedha hizo ama ikibidi akiisoma habari hii katika gazeti la Nipashe awasaidie kwani wanateseka na wanazidi kuwa masikini kwa ujinga wa kutoa ardhi yao na kuipa serikali inayowasumbua.
mwisho
wananchi watakiwa kutoa taarifa za polisi waharifu
Na Gurian Adolf
JESHI la polisi mkoani Rukwa limetoa wito kwa wakazi wa mkoa huo
kutowafichia siri watendaji wa jeshi hilo pindi wanapokuwa wakifanya
vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya kazi yao ili waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo ni pamoja na kutimuliwa kazi.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo Allan Bukumbi
akizungumza na gazeti hili alisema kuwa huu ni wakati ambao si
wakulaumiana ila ni wakila mtu kuwajibika na hivyo kuwataka wananchi
kuacha kulalamika kuhusiana na mwenendo wa watendaji wa jeshi hilo ila
kutoa taarifa hatua ziweze kuchukuliwa.
Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika bila kutoa taarifa
kwa viongozi wa jeshi hilo na kama wanaona kunaudhaifu kwa baadhi ya
askari polisi wanachopaswa kufanya ni kutoa taarifa ili hatua
zichukuliwe.
''tunaomba wananchi wasiogope watoe taarifa kwa viongozi wa polisi
kuhusiana na tabia mbaya za askari, wanaochukua rushwa na walevi ili
tuwawajibishe kwani sisi ndiyo tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa lazima
tuwe waadilifu'' alisema Bukumbi.
Mkuu huyo wa upelelezi wa makosa ya jinai alisema jeshi la polisi
halipo tayari kuchafuliwa na watendaji wake wasiokuwa na maadili ni
bora wakatimuliwa kwani hawafai kuwa sehemu yao kwani sifa za kuwa
mtendaji wa jeshi hilo uadilifu na utii ni sifa za msingi za jeshi
hilo.
Aidha alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kuwa makini katika sikukuu
hizi za Krismas na Mwaka mpya kwa kuwaangalia watoto ambao wamekuwa ni
waathirika wa vitendo vibaya kutokana na wazazi wao kuendekeza starehe
na kuwaacha watoto bila uangalizi wa kutosha.
Alisema nyakati hizi za sikukuu kumekuwa na matumizi ya vilevi kupita
kiasi hali ambayo inasababisha madereva na watembea kwa miguu kupoteza
utashi wawapo barabarani na hivyo kusababisha ajali ambazo zingeweza
kuepukika.

Subscribe to:
Posts (Atom)