Sumbawanga
MKUU wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven amewaambia wafugaji mkoani humo mwenye uwezo wakumuondoa ni rais pekee kwani ndiye aliyempangia akafanye kazi na wala sio wao.
Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika hivi karibuni alisema kuwa wapo baadhi ya wafugaji wanaomchukia kiasi cha kutaka aondoke kwakua amekuwa akiwakamata pindi wanapo kiuka utaratibu wakusafirisha mifugo yao kwani wengine huipitisha kwenye barabara za lami.
Alisema kuwa mara nyingi amekuwa akiwazuia wafugaji kuingiza mifugo yao mkoani humo na wakati mwingine amekuwa akiwakamata yeye mwenyewe kitendo kinachowaudhi nakuona Kama anawanyanyasa.
"baadhi ya wafugaji nimekuwa nikiwakamata mimi mwenyewe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwani wanakiuka utaratibu unaowataka kusafirisha mifugo yao kwa kutumia malori lakini wamekuwa wakikaidi na ninapo wakamata wanaweka chuki kiasi kwamba wanauliza nitaondoka lini"alisema
Alisema hakuna mwenye uwezo wa kumuhamisha mkoa wa Rukwa ama kutengua nafasi hiyo labda rais John Magufuli lakini wao wasahau wanachopaswa kufanya ni kutiisheria kwani hawezi kuwavumilia kwakuwaacha wapitishe mifugo katika barabara za lami zilizojengwa kwa gharama kubwa.
Pia katika kikao hicho mbunge wa jimbo la Kwela Ignas Malocha aliitaka serikali ya mkoa kukabiliana na ma wakala wa pembejeo za kilimo ambao wamekuwa na tabia ya kuwauzia wakulima pembejeo za bandia.
Alisema baadhi ya wakulima wamekuwa wakipata hasara kwa kununua pembejeo za bandia na hivyo kuzidi kuwatia umasikini.
"hivi sasa karibu tunaanza msimu wa Kilimo ni vizuri serikali ya mkoa ikaanza kujipanga kuwadhibiti mawakala hao ili kuwalinda wakulima wasipate hasara"alisema.
Aliwasihi wakulima kuendelea kujituma katika kilimo licha ya malalamiko ya bei ya mazao kuwa ya chini kwani itafika wakati watanufaika na kilimo cha muhimu ni kuto kukata tamaa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment