Wednesday, 23 August 2017

Uhaba wawalimu wa kike wachangia walemavu kuacha masomo

Na Gurian Adolf
Nkasi
IMEBAINISHWA kuwa kutokuwa na walimu wa kike  wa kutosha wanaosomea elimu kwa wanafunzi maalumu nimiongoni mwasababu zinazochangia wanafunzi wa kike wenye ulemavu mkoani Rukwa kuacha shule nakukosa fursa ya elimu hali inayowafanya wazidi kuwa masikini. 

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa maradi wa kupima uelewa wa kielimu unaojulikana kama international aid service ( IAS) Irene Shayo wakati akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo maalumu cha kupima uelewa kwa watoto kilichopo Katika wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. 
Alisema  kuwa kutokana na kutokuwa na walimu wa kike wa kutosha ambao wanawafundisha wanafunzi wenyemahitaji maalumu kumekua kukisababisha wanafunzi hao kuacha shule. 

Shayo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakihudumiwa na walimu wa kiume ambapo wamekuwa wakijidikia vibaya kwani wanafunzi wa kike wanamaumbile tofauti na wakiume hivyo nibusara kuhudumiwa na walimu wa kike  wanapokuwa na shida. 

Alisema kuwa vipo vipindi Katika makuzi ya mwanadamu ikiwepo ni pamoja na Kupata hedhi sasa wamekuwa hawajisikii vizuri kuhudumiwa na walimu wa kiume. 

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kutokana na changamoto hizo zimekuwa zikisababisha wanafunzi hao kuacha shule na kukosa fursa muhimu ya elimu ambayo ingeweza kuwakomboa Katika maisha yao.

Alisema kuwa iwapo kutakuwa kunawalimu wa kutosha kutasababisha wanafunzi hao kusoma kwa uhuru kwani wanajua kua iwapo watahitaji msaada walimu hao wapo nawatawasaidia Katika changamoto zitakazowapata. 

Katika uzinduzi wakituo hicho pia mkurugenzi wa halmashauri  wa wilaya ya Nkasi Julius Kaondo alitoa wito kwa walimu wa kike kusomea elimu hiyo iliwaweze kuwasaidia wanafunzi wa kike wenyemahitaji maalumu kwani walemavu wataendelea kuwepo miaka yote. 

Hata hivyo mkurugenzi huyo aliushukuru mradi huo wa international aid service ( ias) kutekelezwa Katika wilaya hiyo kwani utatoa fursa kwa wanafunzi wenye changamoto mbalimbali kufikiwa na kusaidiwa kuondoka Katika changamoto hizo. 

Pia aliwashukuru wafadhili wa maradi huo ambayo ni serikali ya Denimark pia wakishirikiana na kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT) ambao wanajitolea Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wenyechangamoto wanasaidiwa. 

Mwisho

No comments:

Post a Comment