Na Walter Mguluchuma
Katavi.
SERIKALI imewaonya Watanzania wapya waliokuwa raia wa nchi ya Burundi iwapo watabainika kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ile ikiwemo kufanya mazoezi ya kivita,ujangili,ubaguzi wa kikabila na dini haitasita kuwafutia uraia wao na kuwarejesha Katika nchi walizotoka.
Onyo hilo limetolewa jana na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi , Mwigulu Nchemba wakati akihutubia mkutano wa hadhara watanzania hao wapya wanaoishi katika makazi ya Katumba.
“ Wapo baadhi yenu ambao mmeshakubaliwa na kupewa uraia wa nchi hii zipo taarifa kuwa mnajihusisha na uhalifu ikiwemo ujingili katika hifadhi zetu pia mna ubaguzi wa kikabila ambapo mnawahamasisha wenzenu wasinunue bidhaa kwenye maduka ya wafanya biashara wazawa wa nchi hui... hii hatuwezi kukubali"...alisemaWaziri huyo aliongeza"wenyewe kwa wenyewe mnabaguana kwamba wengine mnatoka milimani na wengine chini ya milima mkidharauliana kuwa upande mmoja ni bora kuliko mwingine huu si utamaduni wetu watanzania “... alisema
Aliwataka wawe raia wema na wazalendo huku akisisitiza kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya kuwapatia uraia ambapo mpaka sasa kuna vyeti vya uraia vipatavyo 7,551 ambavyo havijachukuliwa licha ya wakimbizi walioomba kukubaliwa kuwa watanzania wapya.
Alisema Serikali haiwezi kuondoo utaratibu wa watu kuingia kwenye Makazi hayo bila mtu kuwa na kibali mpaka hapo itakapokuwa imejiridhisha kuwa watu wanao ishi kwenye maeneo hayo watakuwa wameacha vitendo vya uharifu.
Alifafanua kuwa yeye kama Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi hata kubali kuondoa vizuizi vya barabarani kwenye makazi hayo wakati mpaka sasa kuna watu wanaotoka kwenye Makazi hayo wanaendelea kukamatwa katika matukio ya ujangili na uharifu wa aina mbalimbali.
Aidha Serikali imekataa kuwapatia uraia wapatao 3,100 wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi wanao ishi katika makazi ya Katumba na Mishamo Mkoani Katavi ambapo wakimbizi 900 wamekataliwa ni wakazi makazi ya Katumba Wilayani Mpanda huku katika kambi ya Mishamo wilayani Tanganyika ni wakimbizi 1,300 ambao wamekataliwa kutokana na sababu mbalimbali
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Katavi , Raphael Muhuga aliwataka wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo ya Katumba ambao wanataka kurejea Burundi wawe huru kwani milango iko wazi la muhimu wazingatie na kufuata taratibu.Aliwataka raia hao wapya waendelee kutunza mazingira kama ambavyo walivyokuwa wakiyatunza kama kabla ya kuwa raia wa Nchi hii.
Mwisho
No comments:
Post a Comment