Katavi
Baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi wamelalamikia kitendo kilichofanywa na Madaktari bingwa cha kusitisha ghafla na bila taarifa huduma ya upimaji na utoaji wa matibabu ya magonjwa yasiyo ambukiza nakisha kuondoka nakuwaacha bila kuwahudumia.
Madaktari hao wa magonjwa mbalimbali yasiyo ambukiza wa kutoka tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na hospital ya Oceanroad walikuwa wakitoa huduma katika uwanja wa Polisi uliko Manispaa ya Mpanda mkoani humo.
Huduma za upimaji wana utoaji wa matibabu ya magonjwa yasiyoambukizwa ulizinduliwa juma tano ya wiki iliyopita na waziri wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu.
Madakitari hao walikuwa wameletwa Mkoani Katavi kwa ajiri ya kutoa huduma hizo na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani humo Anna Lupembe ambae alipita katika Wilaya zote tatu za mkoa huo na kuwatangazia wananchi na kuwahakikishia kuwa huduma za madaktari hao zitakuwepo hadi siku ya ijumaa lakini zilisitishwa siku moja kabla yaani Alhamisi na kuwasababishia wananchi hasa za gharama kwa wananchi waliokuwa wametoka vijijini.
Mkazi wa Kijiji cha Karema Said Juma alisema yeye ni mmoja wa wakazi wa Tarafa ya Karema aliyesafiri umbali wa kilometa 130 kwa ajiri kufuata huduma zinazotolewa na madaktari hao lakini alipofika kwenye eneo waliokuwa wakitolea huduma alikuta mabanda yako wazi huku kukiwa hakuna daktari bingwa hata moja nawagonjwa wamekaa.
Naye Abel Kalifumu Mkazi wa Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele alieleza kuwa yeye na wenzake walifika Wilayani Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa huduma baada ya Mbunge Lupembe kuwatangazia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya alhamisi katika viwanja vya Mkuu wa Wilaya ya Mlele kuwa huduma itakuwepo mpaka siku ya ijumaa na wakasafiri kesho yake alfajiri lakini walipofika mjini Mpanda walikuta hakuna huduma.
Jojina Katumbo mkazi wa Tarafa ya Mpimbwe alieleza kuwa walitangaziwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika usevya Wilayani Mlele kwenye mkutano huo ambao uliutubiwa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu kuwa huduma hiyo itatolewa mpaka siku ya ijumaa lakini haikuwa hivyo.
Alisema kuwa kitendo hicho kimewasikitisha sana wananchi hao ambao walisema kuwa kama suala likikuwa ni malipo wangewaambia wauze hata mifugo na chochote ilimradi wapate huduma kwani wao kuwahudumia pale gharama ingekuwa nafuu kuliko kuwafuata Dar es Salam ambapo pia ni shida kuwapata.
"Kwaweli kitendo walichotufanyia ni unyanyasaji kanakwamba sisi sio binadamu na hatunahaki ya kutibiwa na madaktari hao....basi acha tu tufe kwakua hatuthaminiki hatuna jinsi kwakua ni masikini"..alisema Moses Kaihero
"kinachotusikitisha nikutufanya tuone mpaka waziri wa afya alietuambia matibabu yapo mpaka siku ya ijumaa lakini wakayasitisha siku ya alhamisi kama nayeye alitudanganya tu,lakini labda kwakua ni mwanasiasa alikua anafanya siasa mpaka kwenye afya zetu"...alisema Richard Kayanda
Hata hivyo taarifa za kutoka ndani ya vyanzo vya habari vinadai kuwa kulikuwa na kutofautiana kwa baadhi ya makubaliano baina ya madaktari bingwa na mwenyeji wao ambaye ni mbunge Lupembe hali iliyopelekea hata mafuta ya gari aina ya basi walilokuwa wakilitumia madaktari hao lilitakiwa kuwekwa mafuta na mbunge huyo wakati wa kuwarudisha Dar es salaam lakini ilibidi yatolewe na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa huo kutokana na tofauti iliyojitokeza.
Mwisho
No comments:
Post a Comment