Na Walter Mguluchuma
Katavi
MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Jackison Eijuel (52) mkazi wa makazi ya wambizi ya Katumba kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 99 baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki na meno manne ya tembo pamoja na vipande vinne vya meno hayo.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Chiganga Ntengwa ,baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka ambapo mshitakiwa hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake.
Akisoma hukumu hiyo hakimu Ntwengwa alisema mahakama imebaini mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria namba 235 cha mwenendo wa mashitaka.
Alisema baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa mahakama imethibisha pasipo kuacha shaka yoyote kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia kwa kukamatwa akiwa na meno ya tembo ambayo ni sawa na waliuawa tembo watatu wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 90.
Awali mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali Fraviani Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Jackisoni Elijuel ambaye alipewa uraia waTanzanja ambapo awal ialikuwa raia wa Burundi alitenda kosa hilo Oktoba 25 mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku katika Kijiji cha Urwila tarafa ya Nsimbo wilayani Mpanda.
Kuendelea kuiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alikamatwa na askari maalumu wa kuzuia ujangili wa pori la Ugala baada ya kuwa walipata taarifa za mshitakiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza meno ya tembo.
Mwendesha mashtaka huyo aliza kuwa baada ya askari hao kupata taarifa hizo ndipo walipoandaa mtego na waliweza kumkamata akiwa na meno ya tembo manne mazima na vipande vinne vyenye uzito wa kiligramu 27 yenye thamani ya shilingi milioni 99 ambayo ni sawa na tembo watatu wazima.
Mshitakiwa katika utetezi wake aliomba mahakama hiyo imwachie huru kwa kile alichodai kuwa meno ya tembo aliyokamatwa nayo hayakuwa yak wake bali yalikuwa ni ya mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Hussen Samora ndie aliyekuwa amemtuma kuyabeba kwa kutumia pikipiki yake mshitakiwa ili ampelekee.
Baada ya utetezi huo kabla ya hakimu kusoma hukumu wakiri wa Serikali Shiyo aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine kwani vitendo vya ujangili vimezidi kushamili katika hifadhi ya Katavi.
Baada ya kuusikiliza utetezi wa mshitakiwa hakimu huyowa alimtaka mshitakiwa ataje namba za pikipiki ambayo alidai ni mali yake aliyoitumia kubebea meno hayo ya tembo na amekuwa akiiendesha kwa kipindi cha miaka miwili hata hivyo mshitakiwa alishindwa kuzitaja namba hizo za pikipiki aliyodai ni ya kwake kitendo kilichothibitisha aliidanganya mahakama kuwa alikodiwa ili pikipiki yake itumike kubeba meno hayo ya tembo.
Akisoma hukumu hiyo hakimu Ntengwa alisema mshitakiwa amekutwa na hatia kinyume na kifungu cha sheria namba 235 ya mwenendo wa mashitaka hivyo mahakama imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 99.
Mwisho
No comments:
Post a Comment