Na Walter Mguluchuma
Katavi
BAADHI ya watanzania wapya wanaoishi katika mkazi ya Katumba wilaya Mpanda katika mkoa wa Katavi wamemuomba Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi iyafute baadhi ya madhebu ya dini yanachoche ubaguzi wa kidini Katika makazi yao.
Ombi hilo waliliwasilisha jana kwa waziri Mwigulu Nchemba wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika makazi ya Katumba.
Mmoja wa wakazi hao Yusuf Shaabani alimweleza waziri Nchemba kuwa ubaguzi wa kidini umekithiri kwenye makazi yao ambapo hata kuoana waumini wa madhehebu tofauti wanakataliwa.
Alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi wa mathehebu wamekuwa wakihubiri chuki dhidi ya dhehebu jingine na hata kudiriki kuwakataza wafuasi wao wasioe muumini wa dhehebu jingine hata kama wawili hao wamependana.
Naye mkuu wa makazi ya wakimbizi ya Katumba Athuman Ingwe alieleza kuwa Makazi hayo ya Katumba yalianzishwa mwaka 1973 huku yakiwa na jumla ya watu 78,201 na kwa sasa raia wapya wakiwa ni asilimia 98 na walibaki bado ni wakimbizi wa nchi ya Burundi .
“Zoezi la kuwahakiki wakimbizi wa nchi jirani wanaoishi katika kambi hii ambao wanaomba uraia limeanza tangu Juni mwaka huu ambapo hadi sasa wakimbizi wapatao 11, 329 ambao ni sawa na kaya 5,134 wamehakikiwa "alisema Ingwe.
Nae Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Richard Mbogo aliiomba Serikali iliondoe eneo la ukubwa wa ekari 145,000 ambalo wanaishi watanzania wapya na wasio raia kutoka kwenye makazi ya wakimbizi Katumba ili lote liwe makazi ya watu.
Mbogo aliomba ufanyike utaratibu wa kuwapatia elimu ya uraia Watanzania hao wapya ili waweze kutambua sheria za nchi na katiba ya Tanzania ili waweze kuzifuata na kuziheshimu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment