Tuesday, 8 August 2017

Wakulima waaswa

Na GurianAdolf 
Sumbawanga
WAKULIMA mkoani Rukwa wameshauriwa kuwa kamwe wasitegemee kupata faida kutokana na kitendo Chao cha kuuza mazao bila kuyasindika kwakua faida inapatikana baada ya kuongezwa thamani kwakusindika. 
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura ambaye alikuwa akimuwakilisha mkuu wa mkoa huo aliwaambia wakulima wa mkoani humo wakati akihitimisha maonesho ya nanenane yaliyofanyika jana Katika kata ya Pito katika Halmashauri ya Sumbawanga. 
Alisema kuwa wakulima wamekuwa wakilalamikia kutopata faida Katika kilimo ni kutokana na tabia ya kuuza mazao bila kuyasindika na daima anayekwenda kunufaika ni mfanyabiashara. 
Binyura alisema kuwa hivi sasa serikali ya awamu ya tano inasisitiza uchumi wa viwanda hivyo basi ni fursa kwao kuhakikisha pia wanawekeza Katika viwanda ili waweze kuuza mazao ambayo yamesindikwa ili waweze kupata faida zaidi. 
Awali akimkaribisha mkuu huyo wa wilaya Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justin Malisawa aliwaasa wakulima kuacha kubweteka wakiwaza pembejeo za luzuku kwani si lengo la serikali kumgawia kila mkulima pembejeo hizo bali zipo kwaajili ya wananchi ambao wanakipato duni. 
Alisema kuwa kitendo cha baadhi ya watu kulalamikia ukosefu wa pembejeo za kilimo ni makosa kwani serikali inatoa mfuko mbegu, na mbolea kwaajili ya hekari moja na kwawatu wasiokuwa na uwezo. 
Naye Pèter kamala mkazi wa mjini Sumbawanga àliiomba serikali kuwachukulia hatua wananchi ambao hawajishughulishi na kilimo kwani ndio ambao wanakuwa kichocheo cha wengine kuwa wavivu na hatimaye kusababisha njaa. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment